Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima aliesimama akitoa ufafanuzi wa
hoja kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira mara
baada ya Kamati kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa
Rais kwa kipindi cha Julai – Desemba, 2018.
Ushauri
huo umetolewa katika kikao baina ya
Kamati hiyo na watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakati wa kuwasilisha
taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi hiyo kwa kipindi cha miezi sita yaani
(Julai 2018 – Desemba 2018).
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti Waheshimiwa Wabunge wameishauri Serikali kuhuisha kampeni
ya upandaji miti katika Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo Vikuu ili kasi ya
upandaji miti iendane na kasi ya ukuaji wake, ikiwa ni pamoja na kutekeleza kwa
vitendo mpango wa kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.
“Wekeni
utaratibu wa kutoa motisha kwa wanafunzi wanaofanya vizuri zaidi katika kupanda
na kutunza miti” alisisitiza Mhe. Dotto Gimbi Mjumbe wa Kamati hiyo.
Akitoa
ufafanuzi mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira,
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima
amesema katika kipindi cha miezi sita, Ofisi ya Makamu wa Rais imepata
mafanikio mengi ikiwa ni pamoja na kutimiza malengo waliojiwekea na kuahidi
kuendelea kuzipatia ufafanuzi changamoto nyingine zilizoibuliwa na wajumbe wa
Kamati likiwemo suala la utekelezaji wa miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya
Tabia nchi kwa upande wa pili wa Muungano.
Vikao
vya Kamati za Kudumu za Bunge vinaendelea katika kumbi za Bunge Jijini Dodoma
na siku ya kesho Kamati hii itapokea taarifa ya Usimamizi na Matumizi salama ya
Bioteknolojia ya Kisasa na Maandalizi ya Mpango wa Taifa wa Kupunguza Matumizi
ya Zebaki kwa Wachimbaji wadogo wa dhahabu chini ya Mkataba wa Minamata.
No comments:
Post a Comment