TANROADS NA JICA WASAINI MKATABA UJENZI WA DARAJA LA GEREZANI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 22 January 2019

TANROADS NA JICA WASAINI MKATABA UJENZI WA DARAJA LA GEREZANI

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe akishuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa daraja la Gerezani kati ya Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads), Eng. Patrick Mfugale (kushoto) na Meneja Mkuu wa Ujenzi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Ichiro Aoki (kulia).

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads), Eng. Patrick Mfugale (kushoto) na Meneja Mkuu wa Ujenzi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Ichiro Aoki (kulia) wakibadilishana hati za mkataba wa ujenzi wa daraja la Gerezani mara baada ya kutia saini jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe akitoa maelekezo kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads), Eng. Patrick Mfugale (kulia) kabla ya kusaini makubaliano ya ujenzi wa daraja la Gerezani jijini Dar es Salaam leo, kati ya Tanroads na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA).

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads), Eng. Patrick Mfugale (kushoto) akisisitiza jambo kwa Katibu Mkuu wa Waziri ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga kabla ya kusaini makubaliano ya ujenzi wa daraja la Gerezani jijini Dar es Salaam leo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe akisisitiza jambo wakati wa hafla ya utiaji saini wa makubaliano ya ujenzi wa daraja la juu eneo la Gerezani jijini Dar es Salaam leo kati ya Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads) na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA).

Sehemu ya wawakilishi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) wakiongozwa na Mwakilishi Mkazi wa JICA Tanzania Bw. Toshio Nagase (kulia), wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe (hayupo pichani) kwenye hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa daraja la Gerezani jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Waziri ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga (katikati) akifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe (hayupo pichani) kwenye hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa daraja la Gerezani jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads), Eng. Patrick Mfugale pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads), Dakta Damas Lucas Nyahoro.  
Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

No comments:

Post a Comment