Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Vijana na Ajira Mh. Antony Mavunde
akizungumza wakati akifunga kilele cha wiki ya Vijana iliyoadhimishwa Jijini
Dodoma kuelekea kilele cha siku ya
UKIMWI inayotarajiwa kuadhimishwa
Novemba Mosi, 2018 Jijini Dodoma.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI Dkt. Leonard Maboko akizungumzia
mambo yaliyofanyika wakati wa kilele cha
shughuli za Vijana kuelekea maadhimisho
ya siku ya UKIMWI Duniani.
Na Mwandishi Wetu
VIJANA Nchini Wameaswa
kushirikiana na Serikalini pamoja na wadau mbalimbali katika mapambano dhidi ya
mambukizi ya virusi vya UKIMWI na kwa kuepuka Tabia hatarishi.
Akizungumza wakati wa
kilele cha wiki ya Vijna kilichofanyika leo Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani itakayoadhimishwa kesho Novemba Mosi 2018, Naibu Waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu, Kazi Vijana Ajira Mhe. Antony
Mavunde amesema kuwa Vijana ni
zaidi ya asilimia 68 ya nguvu kazi ya Taifa hivyo ni vyema kundi hilo
likachukua tahadhari katika kujikinga na maambukizi ya mapya ya VVU.
"Takwimu
zinaonesha kuwa takribani watu elfu 81,000 huambukizwa Virusi vya UKIMWI kila
mwaka hapa nchini, hii ni sawa na takribani watu 6750 kwa mwezi na kwa siku ni
wastani wa watu 225 na katika maambukizi mapya kila mwaka asilimia 40 ni Vijana
wenye umri miaka 15-24"; Alisisitiza Mhe. Mavunde.
Akifafanua Mavunde
amesema kuwa vijana kote nchini wanalo jukumu la kujikinga dhidi ya maambukizi
ya Virusi vya UKIMWI kwa kuwa wanaomchango mkubwa katika ujenzi wa Taifa hasa katika kujenga
uchumi wa Viwanda.
Aliongeza kuwa Nchi yetu imeridhia malengo ya Dunia ya
SIFURI TATU ifikapo mwaka 2030, maana yake ni kuwa ifikapo 2030 tuwe na sifuri
ya maambukizo mapya, sifuri ya vifo vitokanavyo na UKIMWI na Sifuri ya vifo vitokanavyo na
UKIMWI,Sifuri ya unyanyapaa na ubaguzi
kwa WAVIU.
Akizungumzia mwitikio
wa wananchi, Mh. Mavunde amesema kuwa anawapongeza Vijana Jijini Dodoma kwa
kujitokeza kwa wingi kushiriki katika maadhimisho ya wiki ya Vijana na
kushiriki kuzungumzia masuala ya UKIMWI.
Aidha, Mhe. Mavunde
alibainisha kuwa Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI kwa hapa nchini
inasema" PIMA VVU, JITAMBUE, ISHI'' kauli mbiu inatoa msukumo kwa
watanzania kujitokeza kupima VVU kwa hiari baada ya ushauri nasaha.
Tume ya Kudhibiti
UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kwa kushirikina na wadau wanaotekeleza shughuli za
Mwitikio wa UKIMWI, imeratibu maadhimisho ya wiki ya Vijana kuelekea kilelele
cha siku ya UKIMWI Duniani Desemba Mosi 2018 yanayotarajiwa kufanyika Jijini
Dodoma.
No comments:
Post a Comment