Dkt. Charles Mwamwaja Kamishina Masuala ya Fedha Wizara ya Fedha na Mipango akizungumza wakati alipozindua uorodheshaji wa toleo la tatu la hatifungani ya TMRC kwa miaka 5 kwenye soko la hisa DSE.
Bw. Theobald Sabi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TMRC wakati wa hafla ya uorodheshaji wa toleo la tatu la hatifungani ya TMRC kwa miaka 5 kwenye soko la hisa DSE.
Mkuregenzi Mtendaji wa TMRC, Oscar Mgaya akizungumza wakati wa hafla ya uorodheshaji wa toleo la tatu la hatifungani ya TMRC kwa miaka 5 kwenye soko la hisa DSE.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, Nicodemus Mkama akizungumza katika hafla hiyo.
Picha mbalimbali zikionesha baadhi ya waalikwa na wakuu wa vitengo mbaimbali wa TMRC na DSE wakiwa katika hafla hiyo.
Jumoke Jagun-Dokunmu, Mkurugenzi wa IFC kanda ya Afrika Mashariki katikati na Mkuregenzi Mtendaji wa TMRC, Oscar Mgaya wakiwa katika hafla hiyo.
Takriban miaka miwili tangu toleo la pili la hatifungani lilipotolewa na DSE tarehe 1,Julai mwaka 2018 leo ninayo furaha ya kipekee kushiriki leo kwenye uorodheshaji wa toleo la tatu la hatifungani ya TMRC ya miaka 5 kwenye soko la hisa Dar es Salaam DSE.
Tangu TMRC imeanza kutafuta fedha za kukopesha mabenki kwa ajili ya mikopo ya nyumba kwenye soko la fedha nchini shughuli za TMRC zimechangia kwa kiwango kikubwa katika kukua kwa mtaji wa mikopo ya ujenzi wa nyumba hapa nchini.
Hayo yamesema na Dkt. Charles Mwamwaja Kamishina Masuala ya Fedha Wizara ya Fedha na Mipango wakati alipozindua uorodheshaji wa toleo la tatu la hatifungani za TMRC kwa miaka 5 kwenye soko la hisa Dar es Salaam DSE.
Amesema Hatifungani ya TMRC ya miaka mitano ni matokeo ya mpango wa serikali ya Tanzania ya kuongeza upatikanaji wa fedha za muda mrefu chini ya marekebisho ya sekta ya fedha yakiwa na malengo ya kuhakikisha kunakuwa na mpango wa muda mrefu wa upatikanaji wa fedha za muda mrefu zitakazoendana na mahitaji ya soko kwa ajili ya maendeleo ya uchumi wa nchi yetu.
Mikopo ya Nyumba ni eneo muhimu linalolengwa kupitia hatifungani hizi ambazo tumezizindua ili kuendeleza ujenzi wa nyumba kwa lengo la kumpunguzia mwananchi wa chini gharama za ujenzi wa nyumba na kupata nyumba bora zenye gharama nafuu ili kuleta ustawi wa wananchi.
Dkt. Mwamwaja ameongeza kuwa tafiti zinaonesha kwamba kuna uhusiano wa karibu sana mtu anakuwa na utulivu sana pale anapokuwa na makazi bora, mchango wake katika uchumi unakuwa mkubwa sana ndiyo maana serikali iliridhia kuchukua mkopo huu kutoka Benki ya Dunia ili kuwezesha jambo hili kwa ufanisi mkubwa.
"Uwepo wa TMRC umewezesha mabenki kuanza kukopesha mikopo ya nyumba na pia idadi ya benki zinazoshiriki katika utaratibu huu zimeongezeka sana ukilinganisha na kipindi kilichopita,".Amesema Dkt. Mwamwaja.
Mfumo wa mikopo ya nyumba una mchango mkubwa katika uchumi wa nchi na hili limeonekana katika nchi mbalimbali duniani ambazo zina mfumo huu wa muda mrefu na wenye kushirikisha wadau mbalimbali.
Mojawapo ya faida za mfumo huu ni kutoa nafasi ya kuwekeza kwenye nyumba kama sehemu ya kuwekeza mtaji ambazo zinaweza kumsaidia mmiliki kuwa na mapato ya ziada na kuchangia kodi za serikali kutoka kwa mmiliki wa nyumba, Kuinua uchumi wa mmiliki wa nyumba ambapo milki pia ni sehemu muhimu ya mali zisizohamishika ambazo zinaweza kuwa dhamana ili kupata fedha kwenye taasisi za fedha.
No comments:
Post a Comment