RAIS MAGUFULI, WAZIRI MKUU MISRI MADBOULY WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MRADI WA KUZALISHA UMEME MEGAWATI 2100 MTO RUFIJI, DAR - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 13 December 2018

RAIS MAGUFULI, WAZIRI MKUU MISRI MADBOULY WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MRADI WA KUZALISHA UMEME MEGAWATI 2100 MTO RUFIJI, DAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly wakishuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme megawati 2100 katika mto Rufiji kati ya Waakilishi wa Kampuni ya J.V Arab Contractors/El Sewedy Electric kushoto pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Waakilishi wa Shirika la Umeme nchini Tanesco Dkt. Tito Mwinuka wapili kutoka kulia akifatiwa na Mwanasheria wa Shirika hilo Isdori Nkindi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly wakishuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme megawati 2100 katika mto Rufiji kati ya Waakilishi wa Kampuni ya J.V Arab Contractors/El Sewedy Electric pamoja na Wawakilishi wa Shirika la Umeme nchini Tanesco.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly kabla ya tukio la la kihistoria la utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme megawati 2100 katika mto Rufiji ambao utagharimu zaidi ya kiasi cha Shilingi za kitanzania Trilioni 6.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Mazungumzo na kushuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme megawati 2100 katika mto Rufiji. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuonesha picha ya mlima Kilimanjaro Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly kabla ya kumkabidhi zawadi ya picha hio.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na  mgeni wake Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly wakati wakielekea kwenye Ukumbi wa Kikwete Hall kwa ajili ya hafla ya utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme megawati 2100 katika mto Rufiji ambao utagharimu zaidi ya kiasi cha Shilingi za kitanzania Trilioni 6.

No comments:

Post a Comment