BENKI YA NMB KUWAZAWADIA SHILINGI MILIONI 100 WATEJA WAKE! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 11 December 2018

BENKI YA NMB KUWAZAWADIA SHILINGI MILIONI 100 WATEJA WAKE!

Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Boma Raballa akizungumza na wanahabari Dar es Salaam leo (hawapo pichani) kuhusiana na kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata', ambapo wateja wanaofanya malipo mbalimbali kwa kutumia mfumo huo watajishindia fedha taslimu, simu janja pamoja na safari ya kwenda mapumzikoni Dubai. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki na Mauzo wa NMB, Omari Mtiga.

Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Boma Raballa (katikati) akizungumza na wanahabari Dar es Salaam leo (hawapo pichani) kuhusiana na kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata', ambapo wateja wanaofanya malipo mbalimbali kwa kutumia mfumo huo watajishindia fedha taslimu, simu janja pamoja na safari ya kwenda mapumzikoni Dubai. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki na Mauzo wa NMB, Omari Mtiga.

Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki na Mauzo wa NMB, Omari Mtiga (kushoto) akifafanua jambo kwa wanahabari katika mkutano huo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Boma Raballa akifuatilia.

Mkutano na wanahabari ukiendelea Ofisi Kuu za Benki ya NMB, jijini Dar es Salaam leo.

BENKI ya NMB imezinduwa kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata', ambapo wateja wanaofanya malipo mbalimbali kwa kutumia mfumo huo watajishindia fedha taslimu, simu janja pamoja na safari ya kwenda mapumzikoni Dubai.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Boma Raballa alisema katika kampeni hiyo zaidi ya shilingi milioni 100 zitashindaniwa.

Alisema takribani wateja 200 wa NMB ambao watafanya malipo kwa mfumo wa 'NMB Mastercard au 'NMB Masterpass' watakuwa kwenye uwezekano wa kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo ile kubwa ya kujishindia safari ya mapumziko iliyolipiwa kila kitu kwenda Dubai ukiwa na mwenza wako kwa siku nne.

Aliongeza kuwa shindano hilo litaendeshwa kwa miezi miwili  kuanzia leo , huku likiwa na lengo la kuwahamasisha wateja wetu kutumia 'NMB MasterCard' kulipia huduma na bidhaa kwenye vituo vya malipo hayo (POS) au malipo kutumia mtandao (E-commerce). Aidha wateja wa NMB wanaofanya malipo pia kwa kutumia 'NMB MasterPass QR pia wanaingia katika kampeni hiyo.

"Kampeni hii licha ya kuhamasisha matumizi ya malipo kwa kutumia kadi pia imelenga kuwazawadia wateja wetu ambao wanaenda sambamba na safari ya mabadiliko kuingia mfumo wa huduma za kidijitali za kibenki," alisema Raballa.

Akifafanua zaidi alisema kutakuwa na washindi 20 kwa kila wiki ambao watajishindia shilingi 100,000 ndani ya kipindi hicho cha miezi miwili, huku washindi wengine 6 wa mwezi kuibuka na simu janja za kisasa 'Samsung S9+' na mwisho washindi wengine 3 kati yao wawili kujishindia safari ya mapumziko kwenda Dubai iliyolipiwa kila kitu.

Aidha alibainisha kuwa, washindi wa Safari hiyo ya mapumziko wataruhusiwa kwenda pamoja na rafiki mmoja chaguo la mshindi na kulala katika hoteli ya hadhi ya nyota tano Dubai kwa siku 3.

No comments:

Post a Comment