Kaimu Mkuu wa Wateja Wadogo kutoka Benki ya NMB, Salie Mlay (kushoto) akimkabidhi moja ya jezi zilizokabidhiwa Kanali Damian M. Majare(katikati). |
Kaimu Mkuu wa Wateja Wadogo kutoka Benki ya NMB, Salie Mlay (kushoto) akimkabidhi mipira Kanali Damian M. Majare (katikati). |
TIMU za Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) zimepokea msaada wa vifaa vya michezo kwa ajili ya
kuboresha timu zao mbalimbali zinazoshiriki katika Ligi Kuu Bara na michuano ya
mbalimbali ya majeshi.
Msaada huo wenye thamani
ya zaidi ya Sh milioni 10 umetolewa na Benki ya NMB Tanzania, leo Jumatatu jijini
Dar es Salaam na kupokelewa na Kanali Damian M. Majare ambaye ni Kaimu
Mwenyekiti wa Kanda ya Ngome.
Akizungumza katika
hafla hiyo, Kanali Damian M. Majare alisema vifaa hivyo vitawawezesha
kujiimarisha kukabili michuano ya majeshi inayotarajiwa kuanza mapema mwakani.
Kwa upande wake, Kanali
Erasmus Bwegoge ambaye ni Mkurugenzi wa Utimamu wa Mwili, Michezo na Utamaduni
kutoka JWTZ amesema timu zitakazonufaika na msaada huo ni pamoja na timu za
Ruvu Shooting, JKT Tanzania, Green Warriors, Mlale JKT ya Songea, Mgambo
Shooting na baadhi ya timu ambazo zinashiriki Ligi Daraja la Kwanza.
Naye Kaimu Mkuu wa Wateja
Wadogo kutoka Benki ya NMB, ambao ndiyo wametoa msaada huo, Salie Mlay amesema
kuwa wanalenga kuona Timu za JWTZ zikiongeza mwamko katika mashindano
mbalimbali hususan mashindano ya majeshi ili waweze kuliwakilisha taifa
kikamilifu.
Meza kuu ilivyoonekana mbele.
No comments:
Post a Comment