Sehemu ya watoto yatima wa Kituo cha 'Green Pastures' cha Mapinga jijini Dar es Salaam wakipata chakula Kunduchi Beach mara baada ya kujumuika na michezo mbalimbali ya watoto. |
KAMPUNI ya Autopro imejumuika na watoto yatima wa Kituo cha 'Green Pastures' cha Mapinga jijini Dar es Salaam ikiwa ni tukio la kurejesha sehemu ya faida yake kwa wahitaji.
Katika tukio hilo kampuni ya Autopro inayotoa huduma za 'Car service, tires, diagnosis, 3D wheel alignmnent balance, accessories, brakes, suspension, batteries, bushes, autodetailing eneo la Goba mwisho jirani na Banki ya CRDB iliwapeleka Kunduchi Beach watoto wa kituo hicho pamoja na kujumuika katika chakula cha mchana.
Akizungumza katika tukio hilo, Meneja Ufundi wa Autopro, Willbard Gandu alisema waliamua kujumuika na watoto hao kwa pamoja na familia zao ili kuwafariji jambo ambalo ni jema katika jamii.
No comments:
Post a Comment