Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mjini Dodoma, jumatatu tarehe 29 Octoba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mjini Dodoma, jumatatu tarehe 29 Octoba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akimkabidhi muongozo wa utendaji kazi Mwenyekiti wa Bodi ya sukari Tanzania Bi Mwamini Juma Malemi kwenye uzinduzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mjini Dodoma, jumatatu tarehe 29 Octoba 2018.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Prof Kenneth Michael Kitundu Bengesi akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mjini Dodoma.
Na Mathias Canal-WK, Dodoma
SERIKALI imeipa changamoto Bodi ya sukari nchini kutekeleza majukumu
yake kwa weledi ikiwa ni pamoja na kusisitiza kuhuisha uzalishaji wa sukari kwa
wingi ili kuondokana na uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi.
KaMpuni mbalimbali za uzalishaji wa sukari nchini
zimeitikia wito wa Serikali wa kuongeza uzalishaji wa sukari ili nchi iweze
kujitegemea kwa bidhaa hiyo pendwa kwa matumizi ya nyumbani na viwandani na
ziada jambo litalopelekea Bodi ya sukari kusimamia majukumu yake ipasavyo ili
kuondokana na uagizaji wa sukari nje ya nchi.
Kauli hiyo imetolewa Oktoba 29, 2018 na Waziri wa
kilimo Mhandisi Dk. Charles Tizeba (Mb) wakati
akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) hafla iliyofanyika
katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mjini Dodoma.
Waziri Tizeba amemtaka Mwenyekiti wa Bodi ya Sukari nchini Bi Mwamini
Juma Malemi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Prof Kenneth Michael Kitundu Bengesi Kudhibiti sukari inayoingia nchini pasina utaratibu huku akiwataka kusimamia
kwa weledi ufanisi katika uongezaji wa uzalishaji wa sukari nchini.
Aidha, Dk. Tizeba alisema kuwa ufungashaji wa
sukari kwenye ujazo wowote ule kwa kutumia vifungashio vya aina yoyote kama
vile mifuko yenye nembo ya SUPER FINE lazima uzingatie Sheria ya Sukari Namba
26 ya Mwaka 2001 ambayo inazuia ufungashaji wa sukari bila kupata idhini ya
Bodi ya Sukari Tanzania.
Alisema
kuwa kwa mujibu wa Sheria hiyo ni marufuku kufungasha au kuuza sukari nyeupe
kwa kuwa sukari hiyo ni kwa ajili ya matumizi ya viwandani kama malighafi na
sio kwa ajili ya matumizi ya kawaida majumbani.
Alisisitiza
kuwa Mtu yeyote atakayebainika kuvunja Sheria hiyo ya Sukari, atawajibika
kulipa faini ya kiasi cha fedha kisichopungua Shilingi Milioni Kumi
(10,000,000) au kifungo cha miaka mitatu (3) jela au vyote kwa pamoja.
“Kuna
watu wanaolipa kodi ili wazalishe sukari lakini inapoingia sukari ambayo
imepenya kinyemela hata ulinganifu wa soko madukani unakuwa mdogo kwa kuwa
wanaoingiza bila utaratibu wanauza kwa kiasi cha chini kwa kuwa hawana uchungu
wa kulipa kodi”
“Na
hili sio jambo la hiara Bodi ni lazima isimame kidete kubaini mianya yote ya
wafanyabiashara wanaoingiza sukari bila utaratibu,” Alikaririwa Dk. Tizeba
Kuhusu
sukari ya viwandani (Industial Sugar) Dk. Tizeba alisema kuwa, wafanyabiashara
wamekuwa wakiomba kiwango kikubwa cha kibali cha uagizaji wa sukari lakini
serikali ikihakiki kupitia kodi waliyolipa inakuwa haifanani na kiasi
kilichoagizwa.
No comments:
Post a Comment