NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII JAPHET HASUNGA AFANYA KIKAO NA WENYEVITI WA BODI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 6 October 2018

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII JAPHET HASUNGA AFANYA KIKAO NA WENYEVITI WA BODI

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga ( wa pili kulia)  akizungumza na  Wenyeviti wa Bodi  za Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na utalii wakati akifungua  kikao cha kutathimini hatua zilizofikiwa katika ukamilishaji wa taratibu za uanzishwaji rasmi wa Jeshi Usu kilichofanyika jijini Arusha. Wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu  wa Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki. 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kulia)  akifungua kikao cha  Wenyeviti wa Bodi pamoja na Wakuu wa Taasisi  zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na utalii kwa ajili  ya  kutathimini hatua zilizofikiwa katika ukamilishaji wa taratibu za uanzishwaji rasmi wa Jeshi Usu. Wa kwanza kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt. Aloyce Nzuki. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Prof. Abiud Kaswamila pamoja na Kamishna  wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, CP Nsato Marijani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TANAPA.

No comments:

Post a Comment