MAKAMU RAIS AIPONGEZA NMB KUSAIDIA SEKTA YA AFYA KISARAWE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 29 October 2018

MAKAMU RAIS AIPONGEZA NMB KUSAIDIA SEKTA YA AFYA KISARAWE

Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu akiangalia mashine ya Oxygen iliyokabidhiwa na Benki ya NMB kwa kituo cha afya Maneromango wilayani Kisarawe mkoani Pwani. Pia benki ilikabidhi jumla ya mashuka 108, vitanda vya kujifunguliwa, na vitanda vya wagonjwa vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 15. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Serikali wa Benki ya NMB, Vicky Bishubo na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, NMB - Joseline Kamuhanda.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akipokea msaada wa vifaa vya hospitali kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha Biashara za Serikali cha NMB – Vicky Bishubo kwaajili ya vituo vya afya vya Maneromango, Chole na Kirui vya wilayani Kisarawe. NMB ilikabidhi jumla ya mashuka 108, vitanda vya kujifunguliwa, na vitanda vya wagonjwa vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 15. Wa pili kutoka (kulia) ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano NMB, Joseline Kamuhanda.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akiangalia moja ya kitanda cha kujifungulia kilichokabidhiwa na Benki ya NMB kwa kituo cha afya cha Maneromango wilayani Kisarawe mkoani Pwani. Pia benki ilikabidhi jumla ya mashuka 108, vitanda vya kujifunguliwa, na vitanda vya wagonjwa vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 15. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Serikali wa Benki ya NMB, Vicky Bishubo na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa NMB - Joseline Kamuhanda.

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu Hassan, ameishukuru Benki ya NMB kwa kwa kutoa msaada wa mashuka 108, mashine za kupumulia wagonjwa mahututi, vitanda maalum vya kujifungulia, na vitanda vya wagonjwa vyote vikiwa na thamani ya Shilingi Milioni 15 kwenye kituo cha afya cha Maneromango wilayani Kisarawe mkoani Pwani.

Akipokea vifaa hivyo aliushukuru ongozi mzima wa Benki ya Nmb kwa kuendelea kusaidia jamii katika suala zima la afya katika wilaya ya Kisarawe na maeneo mengine hapa nchini.

Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Serikali cha NMB, Bi. Vicky Bishubo juzi alimkabidhi Makamu wa Rais Samia Suluhu msaada huo kwa ajili ya vituo vya afya vya Maneromango, Chole na Kirui vyote vya wilayani Kisarawe.

Makamu wa Rais Suluhu Hassan alipokea msada huo mara baada ya ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara za lami Kisarawe mjini, ikiwa sehemu ya ziara yake ya siku sita ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo katika Mkoa wa Pwani.

No comments:

Post a Comment