Sehemu ya washiriki wa mazungumzo ya amani ya Burundi wakishiriki katika mazungumzo hayo kwenye Hotel ya Ngurdoto Mountain Lodge nje kidogo ya Jiji la Arusha kwa siku. |
Na Ahmed Mahmoud Arumeru
MAZUNGUMZO ya kusaka amani ya Burundi chini ya Msuluhishi wa mazungumzo hayo Rais Mstaafu Benjamini Mkapa yamemalizika leo kwa kupokea ripoti ya vyama vya upinzani na ya serikali ili kuweza kuzipitia na hatimaye kukabidhi kwa Rais Yoweri Museven.
Kikao hicho cha Tano ambacho kimemalizika leo ambacho kiliwashirikisha marais wastaafu ,makamu maraisi,spika mstaafu na wanasiasa mashuhuri, viongozi wa dini, na asasi za kiraia na waandishi wa habari wa nchi ya Burundi kimeenda vizuri chini ya masuluhishi Mzee Mkapa kitakuwa ni ndio njia ya kueleka kwenye amani na uchaguzi mwaka 2020.
Wajumbe waliopo katika vikao vinavyofanyika faraghani wametia saini katika mapendekezo yao kuhusu namna mzozo wa Burundi unavyoweza kupatiwa suluhusu, mpango ambao unantarajiwa kuwasilishwa kwa muwezeshaji Benjamin Mkapa na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Akizungumza na Vyombo vya habari Msaidizi wa Msuluhishi Balozi David Kapya amesema kuwa baada ya kuipitia na kujadili viongozi hao wamemkabidhi msuluhishi ripoti hiyo ambazo atazipitia kwa pamoja na ile ya serikali na kwa haraka ataikabidhi kwa msuluhishi mkuu Rais wa Uganda.
Amesema kuwa anshukuru kwa kiako hicho kuweza kuja na njia nzuri ya kumaliza tofauti zao za kisiasa kwa kukaa kwa pamoja kwa siku tano na kuja na njia agenda hii ambayo wengi aliondoa tofauti zao za kisiasa na kuweka mbele maslahi mapana ya taifa lao
“Sasa hivi msuluhishi ataangalia ripoti za makundi haya ikiwemo ripoti ya Enteber na Kayanza na kuzipitia na baadae atazikabidhi kwa Msuluhishi mkuu ambapo yeye anaona hapa amefikia mwisho ila wakuu wa nchi za jumuiya ndio wenye maamuzi kwani ndio walimtuma kazi hiyo msuluhishi”alisema Balozi Kapya.
Amesema kuwa serikali ya Burundi ina Ripoti yake na vyama vya upinzani vina ripoti yake hivyo itategemea na maamuzi ya msuluhishi baada ya kuipitia na kuikabidhi kwa serikali ndio wenye maamuzi ya mwisho kama mazungumzo yataendelea.
Kwa Upande wake Rais wa chama umoja wa Aman ya maendeleo Burundi (upd)Chauvineau Mugwengezo amesema kuwa madhumuni ya kikao chao ilikuwa ni kukutana na watawala lakini hawakutokea hivyo wameona kikao chao kimeenda vizuri na wanaamini chini ya msuluhishi wa amani Mzee Mkapa fikra zao na mawazo ya umoja yatapelekea kwenda kwenye uchaguzi huru na wa haki mwaka 2020.
Amesema kuwa fikra zilizotolea na wadau hao ambao wamekutana kwa siku sita ni jinsi ya kuendesha uchaguzi na kuona jinsi ya kusahau yaliopita na kuijenga Burundi yanye kuheshimiana na kuheshimu mawazo na misingi ya haki na usawa.
“Hatua hii imetufanya kuona na wapinzani wenzetu ambao hapo kabla hatujawahi kukaa sehemu moja na fursa nzuri kwa maendeleo ya nchi yetu na umoja wetu kama wana burundi”alisema
Aidha kwa upande wake Kiongozi wa FROLINA Joseph Karumba amesema kuwa sehemu kubwa ya agenda ya Enteber ilipitiwa na kuboreshwa na umoja wa upinzani ili kuweza kujadili amani ya kuduma kwa mgogoro wa Burundi si wa leo ni wamuda mrefu.
Amesema kuwa wamefuraishwa na mazungumzo hayo na wanaamini kama yatafanyiwa kazi na viongozi wakuu wa mataifa ya jumuiya amani ya kudumu itapatikana nchi humo ambapo kikao hichi ni muhimu na kizuri sana na kimeonyesha kukusanya fikra za wote
Wakati mkutano wa wanasiasa wa ndani na wale wanaoishi nje kutoka Burundi katika mazunguzo ya kusaka suluhusu ya amani jijini Arusha nchini Tanzania ukielekea kumalizika, wanasiasa hao wamebaini wasiwasi wao kutokana na hatua ya serikali ya Bujumbura kususia mazungumzo hata hivyo wanaimani na viongozi pamoja na msuluhishi kufikia hatua hiyo .
Baada ya vikao vya siku tano, wajumbe katika mazungumzo ya kusaka amani nchini Burundi wametoa mitazamo yao kuhusu kile kinachoweza kufanyika ili kuzua uwezekano wa kufikia kwenye uchaguzi huru na haki nchini Burundi.
Hii imekuja baada ya muwezeshaji katika mazungumzo hayo rais wa mstaafu wa Tanzania, Benjamin William Mkapa kukiri kwamba juhudi zake za kuwaleta pamoja wadau wote katika mzozo wa Burundi zimekwamishwa na serikali ya Burundi.
Ilitarajiwa kuwa kikao kilichoanza Octoba 24 kingelikuwa cha mwisho katika mlolongo wa vikao vya kuwakutanisha wadau wote katika mzozo wa Burundi ulioanza tangu mwaka 2015 baada ya rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
No comments:
Post a Comment