Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), Dk. Agnes Kijazi akizungumza kwenye semina ya TMA iliyoandaliwa maalum kwa waandishi wa habari. |
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), Dk. Agnes Kijazi akizungumza kwenye semina ya TMA iliyoandaliwa maalum kwa waandishi wa habari. |
MAMLAKA ya Hali
ya Hewa nchini (TMA) imesema tathmini zao zinaonesha kwa sasa wananchi wananchi
wengi wamepata mwamko wa kufuatilia taarifa za utabiri wa hali ya hewa jambo
ambalo ni zuri kwani zinasaidia kupunguza madhara yanayoweza kutokea wakati wa
mabadiliko anuai ya hali ya hewa.
Kauli hiyo imetolewa
leo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), Dk. Agnes
Kijazi kwenye semina ya TMA iliyoandaliwa maalum kwa waandishi kuwanoa juu ya
masuala mbalimbali ya hali ya hewa.
Akifafanua zaidi, Dk.
Kijazi alisema tathimini zao zinaonesha wananchi wamekuwa wakifuatilia taarifa
za utabiri wa hali ya hewa tofauti na ilivyokuwa hapo awali jambo ambalo
linasababishwa na viwango vya usahihi wa taarifa zao.
Alisema taarifa za hali
ya hewa zina umuhimu mkubwa sana kwa jamii hasa katika sekta mbalimbali zikiwemo
za Kilimo, afya, miundombinu na zinginezo hasa kuelekea msimu mpya wa utabiri.
"Taarifa za hali
ya hewa ni muhimu sana kwa Jamii katika kila sekta, ukizungumzia uchumi wa
viwanda lazima utahitaji taarifa za hali ya hewa na hata katika sekta zingine kama
vile, Kilimo, Afya, Mifugo, Nishati, Usafiri wa anga, usafiri wa kwenye maji,
usafiri wa nchi kavu, Utalii na Maliasili, elimu na sekta nyingine nyingi,"
alisema Dk. Kijazi.
Aidha aliongeza kuwa wananchi
wengi kwa sasa wanafahamu na kufuatilia utabiri wa hali ya hewa kwa
sababu unawasaidia katika shughuli zao.
No comments:
Post a Comment