KATIBU MKUU KIONGOZI, BALOZI KIJAZI AZINDUWA RASMI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAHANDISI TANZANIA 2018 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 5 September 2018

KATIBU MKUU KIONGOZI, BALOZI KIJAZI AZINDUWA RASMI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAHANDISI TANZANIA 2018

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Kijazi (wa pili kushoto) akipokea tuzo maalum ya Rais John Magufuli toka kwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Eng. Profesa Ninatubu Lema (kulia) aliyopewa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania kutambua mchango wake kuiwezesha bodi hiyo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Tanzania 2018 leo jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Kijazi (wa kwanza kulia) akimkabidhi tuzo maalum mmoja wa watoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julias Nyerere aliyopewa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania kutambua mchango wake kuiwezesha bodi hiyo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Tanzania 2018 leo jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Kijazi (kulia) akihutubia kabla ya kuzinduwa Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Tanzania 2018 leo jijini Dar es Salaam yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.

Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Eng. Profesa Ninatubu Lema (kulia) akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Tanzania 2018 leo jijini Dar es Salaam.

Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania, Injinia Patrick Barozi akiwatambulisha wageni mbalimbali kwenye hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Tanzania 2018 leo jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yaliyoshirikisha wageni kutoka nchi mbalimbali yatafanyika kwa siku tatu yaani Septemba 5 hadi 7, 2018.

Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania , Eng. Profesa Ninatubu Lema (kulia) akimkabidhi tuzo maalum Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Kijazi (wa pili kushoto) iliyopewa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania kutambua mchango wake kuiwezesha bodi hiyo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Tanzania 2018 leo jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Kijazi (wa pili kushoto)

Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Jim James Yonazi na Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba ambao ni moja ya wadhamini wa maadhimisho hayo wakifurahia jambo pamoja na wageni mbalimbali kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Tanzania 2018 leo jijini Dar es Salaam. 

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Kijazi (wa pili kulia) akitoa tuzo mbalimbali kwa washiriki zilizotolewa na Bodi.

Mmoja wa washiriki kutoka mataifa mbalimbali akipokea tuzo maalum toka kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Kijazi kwenye maadhimisho hayo.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Kijazi akisalimiana na wageni mbalimbali mara baada ya kuzindua sherehe hizo za maadhimisho.

Washiriki mbalimbali kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Tanzania 2018.

No comments:

Post a Comment