TTCL YATOA POLE YA MILIONI 25 MAAFA YA KIVUKO CHA MV NYERERE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 28 September 2018

TTCL YATOA POLE YA MILIONI 25 MAAFA YA KIVUKO CHA MV NYERERE

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) limetoa mchango wa pole ya shilingi Milioni 25 kusaidia katika maafa ya ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere iliyotokea wiki iliyopita Kisiwani Ukerewe, Mkoa wa Mwanza. Pichani kulia ni Meneja wa TTCL Mkoa wa Mwanza, Bw. Jalili Bakari kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Tanzania, Ndugu Waziri Kindamba akikabidhi nakala ya hundi ya malipo hayo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela akishuhudia.

Meneja wa TTCL Mkoa wa Mwanza, Bw. Jalili Bakari kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Tanzania, Ndugu Waziri Kindamba akizungumza mara baada ya kukabidhi nakala ya hundi ya malipo ya mchango wa pole ya shilingi Milioni 25 iliyotolewa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) ikiwa ni pole yao kwa maafa ya ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere iliyotokea hivi karibuni kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela akishuhudia.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela katikati akishukuru mara baada ya kupokea pole hiyo ya shilingi Milioni 25 kusaidia katika maafa ya ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere.

No comments:

Post a Comment