Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam
MKURUGENZI wa Mafia Boxing Promotion, Ally Zayumba amesema pambano lisilokuwa la ubingwa la
Knockout ya Mama msimu wa tatu litafanyika Februari 28, mwaka huu jijini Dar es
Salaam kati ya Bondia Amir Matumla dhidi ya Paulus Amavila kutoka Namibia likiwa na lengo la kutangaza kazi kubwa iliyofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutekeleza miradi mbalimbali nchini.
Zayumba ameyasema
hayo leo Februari 25, 2025 wakati wa mkutano na waandishi wa habari alipokuwa akitangaza
mapambano hilo ambalo litakuwa la raundi nane uzito wa super weight.
“Kutokana
na maandalizi mazuri tunaimani bondia wetu Matumla ambaye ni mtoto wa wa bondia
wa zamani Rashid Matumla atatuwakilisha
vema kwa kufanya vizuri,” alisema Zayumba.
Zayumba
alisema kuwa Amir Matumla katika pambano hilo dhidi ya MnaMIbia huyo ni pambano
lake la kwanza tangu ajiunge kwenye mapambano ya ngumi za kulipwa na ambapo
ametuahidi kuwa atafanya vizuri.
"Tumekaa
naye tumezungumza naye na moja ya malengo yake alituambia tumtafutie pambano la
kimataifa kwa hiyo litakuwa pambano lake la kwanza kwake la kimataifa,"
alisema.
Zayumba
ameongeza kwamba siku ya pambano hilo kutakuwa na mapambano mengine 11 ya
utangulizi yakiongozwa na mkongwe Dullah Mbabe, Abdallah Pazia, Oscar Richard
na Yohana Mchanja na kueleza kwamba huu ni msimu wa tatu kwa mapambano ya aina hiyo kufanyika
chini ya Mafia Boxing Promotion yakiwa na lengo la kunadi miradi iliyotekelezwa
na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande
wake Amir amesema:" Nashukuru sana Mafia kwa kunipokea, naahidi Watanzania
nitaendeleza kwa ukubwa zaidi, sasa hivi naendelea na mazoezi, watu waje kwa
wingi watafurahi zaidi
Zayumba alitaja viingilio katika pambano hilo kuwa
ni Sh. 50,000, 20,000 na sh 10,000.
No comments:
Post a Comment