Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akijibu maswali katika kikao cha Bunge Jijini Dodoma. |
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
SERIKALI imesema kuwa itaendelea kupeleka fedha za ruzuku katika Halmashauri zote nchini kutokana na makusanyo halisi kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato.
Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu maswali ya Mbunge wa viti maalum, Mhe. Leah Jeremiah Komanya aliyetaka kujua ni lini Serikali itaanza kupeleka fedha za ruzuku katika Halmashauri za wilaya kama zilivyopitishwa na Bunge.
Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alieleza kuwa kinachoidhinishwa na Bunge ni makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka husika na utekelezaji wake kwa sasa unafanyika kwa mfumo wa kutumia kile kinachopatikana ‘cash budget’.
Dkt. Kijaji alisema kuwa ruzuku kutoka Serikali Kuu hupelekwa kwenye Halmashauri za wilaya kulingana na makusanyo halisi ya mapato ya mwezi husika.
No comments:
Post a Comment