Mwenyekiti wa CHADEMA, Taifa, Freeman Mbowe. |
Na Ahmed Mahmoud Arusha
MAFIWANI nane kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema) wamejiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka wilaya za Monduli, Karatu, Arumeru na Arusha Jiji.
Wakizungumza jana mara baada ya kupokelewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Lootha Sanare, Katibu wa Ccm Mkoa, Mussa Matoroka pamoja na viongozi wengine wa Chama akiwemo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya NYC, Awaki Daniel.
Wakizungumza jana mara baada ya kupokelewa madiwani hao kutoka Chadema akiwemo Diwani wa Kata ya Endamaghan iliyopo Wilayani Karatu, Ally Lorry na Alex Marti wa Olasiti alisema yeye pamoja na madiwani wenzake wamehama chama kutokana na jinsi serikali inavyofanya kazi kwani mabadiliko waliyokuwa wakiyataka serikali ya CCM inayafanyia kazi.
Naye Diwani Alex Marti kutoka Kata ya Olasiti alisema wamerudi nyumbani sababu serikali inafanya kazi nzuri hivyo hawaoni sababu ya malumbano kati yao na serikali.
Nao baadhi ya madiwani wengine waliohama chadema na kurudi CCM ambao ni Yotam Manda(Karatu), Diwani wa Kata ya Engutoto, Amani Liwadi, Arumeru wawili, Longido mmoja na Monduli Mjini mmoja.
Naye Katibu wa Ccm Mkoa wa Arusha, Musa Matoroka alisema mpaka sasa madiwani 37 wamehama kutoka Chadema kurudi CCM huku madiwani 29 kutoka Kata mbalimbali walishinda kwenye uchaguzi wa udiwani na kata nane zinasubiri uchaguzi kufanyika baada ya kuhama vyama vyao.
Naye Mnec, Hawakii kutoka Karatu alisema kuwa Chadema wanapata tabu hivi sasa kwani madiwani wao wanarudi ccm nahadi 2020 upinzani utakuwa umeisha Mkoa wa Arusha.
Awali Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Lootha Sanare alisema hakuna diwani yoyote anayenunuliwa na CCM bali wanarudi CCM kutokana na serikali kufanya kazi nzuri na kuwasihi wanamonduli kuhakikisha wanaichagua CCM inayotekeleza ilani ya chama na wananchi kupata maendeleo.
No comments:
Post a Comment