Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, akifafanua jambo kwa Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka wakati
alipofanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Maswa-Bariadi yenye urefu
wa KM 49.7 kwa kiwango cha lami, Mkoani humo.
UJENZI unaondelea wa barabara ya Maswa-Bariadi yenye urefu wa Km 49.7 kwa kiwango cha lami unatarajiwa kufungua mkoa wa Simiyu na mikoa jirani ya Mara, Mwanza na Shinyanga hivyo kutarahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack
Kamwelwe mkoani Simiyu wakati akikagua barabara hiyo inayojengwa na mkandarasi
wa kampuni ya CHICO na kuridhishwa na hatua zilizofikiwa katika ujenzi huo toka
ulipoanza mwezi Oktoba mwaka 2017.
"Nimeridhishwa
na hatua zilizofikiwa na nina imani mkandarasi atamaliza mapema mradi huu",amesisitiza
Waziri Kamwelwe.
Aidha,
ameupongeza uongozi wa mkoa huo na Wakala wa Barabara (TANROADS), kwa kusimamia
mradi huo usiku na mchana na kuwataka kutoa taarifa muda wowote endapo kutakuwa
na changamoto zinazoweza kukwamisha mradi huo.
Akizungumzia
kuhusu Kiwanja cha Ndege cha Simiyu, Mhandisi Kamwelwe amemueleza Mkuu wa
Mkoa kuwa hatua za awali zinaendelea
katika kuhakikisha kiwanja hicho kinajengwa ili kufungua mkoa huo katika sekta
za usafirishaji na uwekezaji.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, ameishukuru Serikali kwa
kujenga kipande cha barabara hiyo baada ya ile ya Mwigumbi-Maswa kukamilika kwa
kiwango cha lami kwa kuwa imekua ni kichocheo cha kuunganisha nchi yetu na nchi
za maziwa makuu ambazo ni Uganda, Burundi, Rwanda, Kenya na Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo(DRC).
Naye,
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Simiyu Mhandisi Albert Kent amemueleza Waziri huyo
kuwa mradi huo mpaka sasa umefikia asilimia 20 na unatarajiwa kukamilika
ifikapo mwezi Oktoba mwaka 2019.
Mhandisi
Kent ameongeza kuwa kazi zilizofanyika mpaka sasa ni mkandarasi kuanza ujenzi
wa madaraja makubwa mawili ya Banhaya na Simiyu na ameshamaliza kujenga
madaraja madogo 9 kati ya 12 na makalvati 36 kati ya 58.
Mradi
wa Maswa-Bariadi unagharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwa asilimia 100 na unatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi Bilioni 86. Kukamilika
kwa mradi huo kutakamilisha ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa-Bariadi-Lamadi
yanye jumla ya urefu wa KM 171.8.
No comments:
Post a Comment