Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dk. Agnes Kijazi. |
Na Ahmed Mahmoud, Arusha
SHIRIKA la Hali ya
Hewa Duniani (WMO) kwa kishirikiana na Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA)
wameandaa mafunzo kwa nchi 23 za Afrika ya utumiaji wa mfumo wa Teknolojia ya
kuboresha huduma za utabiri wa hali ya hewa ambao utasaidia kujua maeneo
yasiona vituo.
Akizungumza jana
Jijini hapa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dk. Agnes
Kijazi wakati wa ufunguzi wa warsha ya mafunzo hayo, alisema mfumo huo
utawezesha utoaji wa taarifa sahihi zahali ya hewa .
Alisema kuwa mbali na
kuboresha utoaji wataarifa pia wataweza kubaini maeneo ambayo hayana vituo na
kuweza kuongeza kwa ajili ya kutoa taarifa zenye uhalisia.
Dk. Kijazi alisema
mafunzo hayo yamekuja mahususi nchini kwa ajili ya kuwanoa wataalamu wa nchi za
Afrika ili waweze kutumia mfumo huo vema.
"Kwa mfano hapa
Tanzania tuna vituo vya aina nyingi kama vya rada tunavyo viwili tunahitaji
saba na Vituo vinavyojiendesha vyenyewe 36 katika mikoa mbalimbali
ikiwemo Arusha, lakini kama nchi tunahitaji kama 100,"alisema
Alisema pia kwa upande
wa vituo vya upimaji wa mvua tunavyo 300 lakini mahitaji ni 2500,hivyo
uhitaji mkubwa na kwa kutumia mfumo huo mpya wataweza kuongeza vingine
zaidi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa
Arusha Mrisho Gambo alisema mafunzo hayo ni muhimu,kwani yanawezesha wataalamu
kubaini hali halisi ya mabadiliko ya tabia ya nchi na jinsi ya kukabiliana nayo
na hivyo kuongeza tija na katika utendaji wataasisi hiyo.
Amesema kuwa hapa
nchini na mkoa wa Arusha kumekuwa na mabadiliko ya Tabianchi hususani maeneo ya
longido ambapo serikali imekuwa ikisaidia kwa karibu katika kuhakikisha masuala
yote yanaenda sawa katika suala zima la kupambana na mabadiliko hayo.
"Taarifa za hali
ya hewa ni muhimu kwa wananchi ili waweze kufanya uamuzi sahihi kwa
shughuli zao mbalimbali," alisema.
No comments:
Post a Comment