Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro. |
Na Ahmed Mahmoud Arusha
SERIKALI imewataka watafiti katika nchi za jumuiya ya Afrika mashariki kuangalia namna ya kuzipatia matokeo tafiti zinazofanyika katika nchi zao badala ya sasa kuishia kwenye makabati na kushindwa kutoa matokeo chanya.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakati akifungua mkutano wa wataalamu wa sekta ya utafiti kutoka nchi za Afrika Mashariki (EARIMA) unaofanyika kwa siku tatu jijini hapa.
Amesema kuwa ilikufikia malengo ya uchumi wa kati wa viwanda Tafiti ndio dira ya kutufikisha huko kwani bila jitihada za serikali kuongeza fedha katika Tafiti na kutoa matokeo chanya hatutafika tunakohitaji.
Amewataka Watafiti hao kungalia zaidi majibu na kuongeza wigo utaoleta tija katika tafiti ndio maana serikali ya awamu ya Tano inatoa fedha nyingi kwa ajili ya Tafiti ili kufikia uchumi wa kati wa viwanda.
"Mkifanya tafiti muangalie jinsi ya kutoa matokeo chanya yatakayoasaidia mataifa yetu kuzalisha bidhaa kwa tija na kuachana na tafiti kuishia kwenye makaratasi bila kutoa muelekeo utakaosaidia nchi zetu kufikia uchumi wa kati wa viwanda," alisisitiza DC Muro.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa wataalamu wa utafiti (EARIMA) Tanzania Dk. Alfred Sebahene amesema kuwa mkutano huo wa mwaka huu utakuja na namna bora ya kuongeza wigo mpana utakaosaidia kuleta matokeo chanya yatakao saidia malengo ya serikali kufikia uchumi wakati kwa nchi zetu za Afrika mashariki.
Amesema kuwa Mataifa hayo ya Afrika mashariki yamelenga kuongeza utafiti utaoenda mbele kutoa matokeo yenye tija kuweza kusaida uchumi wetu tofauti na huko nyuma kuishia kwenye makaratasi.
"Tunaenda kuangalia namana nzuri ya kuyasaidia mataifa yetu kujikwamua na hali duni ya kufikia uchumi wa kati kwa kutoa tafiti zenye matokeo chanya zenye kufikia malengo tarajiwa," alisema Dkta Sebahene.
No comments:
Post a Comment