HALOTEL YAWAFURAISHA WANAKIJIJI ARUMERU KWA KUPELEKA MAWASILIANO YA UHAKIKA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 28 August 2018

HALOTEL YAWAFURAISHA WANAKIJIJI ARUMERU KWA KUPELEKA MAWASILIANO YA UHAKIKA


Mwenyekiti wa Kijiji cha Timbolo Halmashauri ya Wilaya ya Arusha DC, Samwel Kivuyo, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) waliotembelea kijiji hicho kuangalia miundombinu ya mawasiliano iliyowekwa na Kampuni ya Halotel. Kushoto ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Josephine Mhina.

WAKAZI wa kijiji cha Timbolo,Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, wamepongeza jitihada za mtandao wa simu wa Halotel kwa kufikisha mawasiliano kijijini hapo baada ya kuhangaika kwa muda mrefu kupata huduma za Mawasiliano ya uhakika jambo ambalo limechangia kwa ukuaji wa shughuli za kiuchumi kwa wakazi wa kijiji hicho hususani huduma jumuishi za fedha(financial inclusion).

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa kijiji hicho, Bw. Samwel Kivuyo,  alipokuwa  akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali walipokwenda kutembelea katika kijiji hicho ili kuona na kujifunza shughuli mbalimbali za kimaendeleo ambazo zimechangiwa na mtandao huo kuwekeza katika maeneo ambayo awali hayakuwa na huduma za mawasiliano ya  uhakika.

‘’Halotel wamesaidia sana kufikisha huduma jumuishi za kifedha kwa wananchi masikini wa kijiji hiki ambao awali walikuwa wanataabika na kupitwa na huduma hizo hivyo kulazimika kutembea kilometa nyingi kufuata huduma za kifedha,kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kijiji hicho, Bw. Samwel Kivuyo.

Baadhi ya wanakijiji wa kijiji hicho katika kata ya Sambasha,wameelezea kufurahishwa na huduma ya Halopesa,ambapo wamesema,imekuwa rafiki kulinganisha na huduma kama hizo zinazotolewa na kampuni nyingine,kufutia Halotel kutotoza makato pindi mtumiaji wa huduma hiyo akituma pesa kwenda mtandao huo.

“ Kwakweli ukiwa na huduma za Haloteli,unafurahia kupata muda wa maongezi wa kutosha,data ndiyo siwezi kuelezea,yaani ni huduma rafiki sana kwa sisi hasa wa huku kijijini ambao kipato chetu ni cha chini. Alisema,Rehema Joshua,mkazi kijiji cha Timbolo,kata ya Sambasha,Wilaya ya Arumeru,mkoa wa Arusha.
"Sisi kama wananchi wa Timbolo tunashukuru kwanza kabisa jitihada za serikali kwa kuiwezesha kampuni ya  Halotel  kuweza kuweka minara ya mawasiliano katika kijiji chetu ili wananchi waweze kupata huduma za mawasiliano katika maeneo yao na kusaidia wananchi kutumia huduma za mawasiliano katika kujiendeleza kiuchumi kwani hapo awali hatukuwa na huduma ya mawasiliano ya uhakika.,"
   
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda (katikati), akiwaelekeza wakazi wa Kijiji cha Timbolo namna ya kutumia huduma za mtandao wa Halotel wakati wa ziara ya waandishi wa habari kutembelea miundombinu ya kampuni hiyo.

Mpaka sasa hali ya mawasiliano katika kijiji chetu ni nzuri, watu wamepata ajira kufuatia kuanzisha biashara za huduma za kifedha kwa njia ya simu pamoja na kuongeza uzalishaji wa mazao ya mboga mboga ambayo ni kazi kuu ya wanakijiji wetu, kwani mara ya kwanza mawasiliano na wafanyabiashara wengine yalikuwa ni magumu ila sasa tuna uhakika wa wateja kwa sababu tunawasiliana nao moja kwa moja na hata upokeaji wa malipo umekuwa ni rahisi. Alisema Kivuyo na kuongeza.

"Tunafurahi sana kuwa na mradi wa mawasiliano katika kijijj chetu kwa sababu  miundo mbinu ya mawasiliano iliyojengwa na Halotel .Katika kijiji chetu imesaidia wananchi kuimarisha usalama katika maeneo mbalimbali ya kijiji chetu kwani imekuwa rahisi kupeana taarifa mbalimbali katika kijiji chetu. Alisema

Aidha Mwenyekiti huyo alibainisha kuwa hadi sasa changamoto inayowakabili kijijini hapo ni Ukosefu wa umeme katika kijii hicho jambo ambalo linatatiza shughuli za maendeleo kwa baadhi ya wananchi.

“Tunaomba Wakala wa umeme vijijini(REA) watusaidie kupata umeme hasa katika kitongoji cha Meduti  na Murerian ili wananchi waweze kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo na kijamii,ikiwemo  kilimo, uchomeleaji wa vyuma,  shuleni, vituo vya afya ili wananchi waweze kuboresha maisha yao na kujiongezea  kipato katika kijiji hicho kilichoanzishwa mwaka 1972 chenye  wakazi 4638 na jumla ya kivitongoji vinne ambavyo  ni  Oltingidi, Madukani, Meduti na Muterian”,alisema mwenyekiti huyo.

Baada ya kuzungumza na mwenyekiti huyo wa kijiji cha Timbolo,kuhusiana na kadhia hiyo ya umeme,waandishi  walimtafuta mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro,kutaka kufahamu  namna serikali inavyoweza kuwasadia wananchi hao,ambao tayari wameshafanya jitihada za kufungiwa mfumo wa umeme majumbani mwao.

“Kwakweli nawapongeza wananchi hao wa kijiji cha Timbolo,kwa jitihada zao na serikali inafurahishwa mno na ana ya wanachi wanaopenda kujiletea wenyewe maendeleo,na nimemtaka mwenyekiti wa kijji cha Timbolo, Samwel Kivuyo,aje wakati wowote ofisni kwangu akiwa na wawakilishi watatu wa wanakijiji waje tuzungumze na kumaliza mara moja kadhia hiyo ya umeme”,alisema,mkuu wa Wiayaya Arumeru, Jerry Muro.

Wakati huo huo mkuu wa  Idara ya Mawasilianno,Kampuni ya Halotel Tanzania, Mhina Simwenda alisema kuwa kampuni ya Halotel Tanzania ipo mkoani Arusha kwa ajili ya kuongea na wateja,kusikiliza maoni kutoka kwao, kujua wanahitaji nini, kujua changamoto  walizonazo  ili waweze kuboresha huduma zao kwa wateja.

"Ukiangalia kijiji cha Timbolo ndiyo chenye mafanikio mazuri katika suala la mawasiliano na sisi kama Halotel Tanzania tunaishukuru serikali ya kijiji cha Timbolo kwa kuunga mkono juhudi za kampuni yetu ili tuweze kuleta huduma za mawasiliano hapa kijijini," alisema, Semwenda.

No comments:

Post a Comment