Diwani wa kata ya Shirimatunda katika Manispaa ya Moshi, Fransic Shio (CHADEMA) akizungumza wakati wamkutano wa kata uliolenga kujadili masuala ya maendeleo pamoja na kutambulisha wajumbe wanaounda kamati ya maendeleo ya kata hiyo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi akizungumza katika mkutano wa kata ya Shiriamtunda ambapo yeye amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya kata hiyo.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na viongozi.
Naibu Meya wa Manispaa ya Moshi na Diwani wa kata ya Njoro, Jomba Khoi akizungumza katika mkutano huo ambapo yeye na madiwani wenzake walifika kumuunga mkono Diwani wa kata hiyo katika kuchangia shuhghuli za maendeleo.
Baadhi ya wananchi waishio kata ya Shirimatunda wakiwa katika mkutano huo.
Diwani wa kata ya Kiboriloni, Frank Kagoma ni miongoni mwa madiwani walifika kuhamsisha shghuli za maendeleo katika kata ya Shrikamtunda.
Baadhi ya wawananchi waliofika katika mkutano huo.
Diwani wakata ya Soweto, Collins Tamimu pia ni miongoni mwa Madiwani waliofika katika mkutano huo.
Baadhi ya wananchi waishio katika kata ya Shirimatunda.
Diwani wa kata ya Ng'ambo katika manispaa ya Moshi, Genesis Kiwhelu akiwa mmoja wa madiwani waliofika kuhamisisha shughuli za maendeleo katika kata hiyo.
Baadhi ya wananchi wakichangia hoja mbalimbali wakati wa mkutano huo ikiwemo ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa darasa kwa ajili ya shule ya awali katika kata hiyo.
Na Dixon Busagaga
MADIWANI wanne kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika manispaa ya Moshi pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kilimanjaro Patrick Boisafi wamejitokeza kumuunga mkono Diwani wa kata ya Shirimatunda, Francis Shio (Chadema) kuhamasisha uchangiaji katika shughuli za maendeleo.
Madiwani waliojitokea katika mkutano maalumu wa Diwani kata na wananchi wa kata hiyo, ni pamoja na Diwani wa kata ya Soweto, Collins Tamimu, Diwani wa kata ya Njoro na Naibu Meya wa manispaa ya Moshi, Jomba Khoi, Diwani wa kata ya Ng’ambo Genesis Kiwhelu na Diwani wa kata ya Kiboriloni, Frank Kagoma.
Akizungumza wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ofisi ya kata ya Shirimatunda ,Diwani wa kata ya Shirimatunda ,Fransic Shio alisema maendeleo ya wananchi katika maeneo yao yataletwa na wananchi wenyewe na si itikadi za kisiasa kama baadhi ya wanasiasa wanavyoamini.
“Shirimatunda yetu ni ya kwanza kuliko vitu vingine,haya ninayo yasema ni ya uwazi tukikubali kuyaingiza mambo ya kisiasa katika maendeleo ya kata yetu ,yapo mambo mengi sana yatasimama ,ni lazima kaul yetu ya wana Shirimatunda,umoja ya wana Shirimatunda na amani yetu tuweze kuilinda kwa gharama yoyote”alisema Mh Shio.
Shio aliwataka wakazi wa Shirimatunda kuwaondoa katika misingi ya umoja wa wakazi wa kata ya Shirimatunda huku akiwaomba kupitishwa azimio la kuchangisha fedha kwa kila familia katika kata hiyo kutoa kiasi cha Sh 10000 kwa ajili ya ujenzi wa darasa la wanafunzi wa shule ya awali.
Kwa upande wao ,Madiwani waliofika kumuunga mkono Diwani huyo,walisema ili kushawishi wadau mbalimbali pamoja na serikali kujitokeza kuchangia maendeleo katika kata hiyo wakazi wa eneo hilo wanapaswa kuwa wa kwanza katika kuchangia.
“Mgeni akija nyumbani akakuta wewe mwenyewe hujielewi ,hata kama amekuja na zawadi atarudi nayo ,watu wa Shirimatunda wanaangaliana nani anatoa nini ,endapo kila mkazi wa Shirimatunda akiguswa na hiki tunachokifanya basi angechangia katika eneo hili la elimu”alisema Diwani Kagoma.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia amechaguliwa kuwa mwenyekiti ya maendeleo ya kata hiyo ,Patrick Boisafi alisema kuchangia ujenzi wa Madarasa kwa wanafunzi wa elemu ya awali ni jambo la Kihistoria katika kata hiyo.
“Hakuna mashamba tena hata ya kuwagaiwa watoto wetu ,shamaba lililobaki ni moja na la muhimu sana ambalo ni Elimu,kuna watu ambao wamekuja hapa kutuunga mkono wakasema wafanye jambo ambalo litaacha Historia na ni hili la kuchangia shule ya awali name naunga mkono jambo jema kama hili “alisema Boisafi.
Kwa upande wake ,Naibu Meya wa Manispaa ya Moshi na Diwani wa kata ya Njoro alisema Halmashauri itatoa kipaumbele katika ujenz wa Madarasa hayo kwa kutenga Fungu hasa kutokana na hamasa walioyoionesha wakazi wa kata ya Shirimatunda kw akuanza kuchangia.
“Niliwaambia nimekuja kujifunza kutoka kwenu na nimeona jinsi mlivyo weza kuanzisha michango na kuonyesha mahitaji yenu kwamba shule ya awali imeonekana kuwa kipaumbele ,ni lazima na mimi kwenye halmashauri yangu tutaipa kipaumbele tutatoa Sh Mil 10 kwa mwaka wa fedha ujao wa 2018/2019.”alisema Khoi.
Katika hatua nyingine wananchi wa Kata hiyo wameiomba serikali kupitia Wakala wa Barabara vijijini na Mjini (TARURA) pamoja na Halmashauri ya manispaa ya Moshi kutoa kipaumbele cha barabara kwa kata hiyo ambayo haina kipande hata kimoja cha barabara ya Lami.
No comments:
Post a Comment