Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakiadhimisha Siku ya Mashujaa kwa kufanya usafi katika eneo la Coco Beach jijini Dar es salaam Julai 25, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). |
WAZIRI Mkuu, Kassim
Majaliwa Julai 25, 2018 anatarajiwa kushiriki zoezi za usafi eneo la Coco Beach
pamoja na wananchi na watendaji mbalimbali.
Zoezi hilo ni
utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John
Pombe Magufuli alilolitoa Juni 29 mwaka huu kwamba Watanzania wafanye usafi
kwenye maeneo yao ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya
Mashujaa ambayo huadhimishwa Julai 25, kila mwaka.
Kwa muhibu wa ratiba
iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, wananchi wanatakiwa wafike
eneo hilo kuanzia saa 12:30 asubuhi ili waanze shughuli hiyo. Usafi huo
utafanyika kuanzia kwenye eneo la wafanyabiashara wa mihogo kuelekea maeneo ya
Police Officers’ Mess.
Juni 29 mwaka huu,
wakati akitoa maelekezo kwenye hafla ya uzinduzi wa kituo cha polisi
kinachohamishika, Waziri Mkuu alisema: “Rais Dkt Magufuli anawataka Watanzania
wote waadhimishe siku hiyo ya kumbukumbu ya mashujaa kwa kufanya usafi
katika maeneo yaliyo jirani na makazi yao pamoja na yale ambayo wamezikwa
mashujaa ikiwa ni njia ya kuwaenzi.
Siku hiyo hiyo, Waziri
Mkuu alitangaza kwamba Rais Magufuli ameagiza kwamba sh. milioni 308 zilizotengwa
kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa, zitumike kuboresha
miundombinu ya barabara jijini Dodoma.
Aliitaja miundombinu
hiyo ni pamoja na taa za kuongezea magari katika barabara ya Kisasa na taa za
barabarani kwenye barabara mpya ya kutoka Emmaus hadi African Dream yenye urefu
wa kilomita 1.4, ambayo kwa sasa inajengwa kwa kiwango cha lami.
No comments:
Post a Comment