WATAALAMU WA UBIA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR WAJADILI UBIA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 5 February 2026

WATAALAMU WA UBIA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR WAJADILI UBIA

Mchumi Mkuu kutoka Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPU), Wizara ya Fedha, Bi. Josephina Melkiol Buhili, akitoa wasilisho wakati wa kikao cha wataalamu wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) kutoka Wizara yaa Fedha, Tanzania na Wizara ya Kazi na Uwekezaji Zanzibar, kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar Es Salaam.

Wataalam wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi kutoka Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPU), Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), pamoja na Wataalamu kutoka Idara ya Ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPD), Wizara ya Kazi na Uwekezaji- Zanzibar, wakifuatilia wasilisho la Mchumi Mkuu kutoka Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPU), Wizara ya Fedha, Bi. Josephina Melkiol Buhili (hayupo pichani) wakati wa kikao kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar Es Salaam.

Na Asia Singano, WF, Dar Es Salaam

WATAALAMU kutoka Kitengo cha Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), na Wataalam kutoka Wizara ya Kazi na Uwekezaji, Zanzibar, kupitia Idara ya Mashirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPD), wamekutana na kujadili kuhusu maandalizi ya Kikao cha Kwanza cha Ushirikiano kati ya pande zote mbili kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar Es Salaam.

Katika kikao hicho wataalamu hao walijadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupitia na kuthibitisha ajenda zitakazojadiliwa katika Kikao cha Kwanza cha Ushirikiano huo.

Wataalamu hao pia walipitia taarifa ya utekelezaji wa yatokanayo na kikao cha pili cha Ushirikiano kwa mwaka wa fedha 2024/2025, na kupata wasilisho kuhusu Rasimu ya Mwongozo wa Usimamizi wa Misaada ya Kibajeti na Madeni Sanjari.

No comments:

Post a Comment