MAKAMU WA RAIS AKABIDHI TUZO ZA MZALISHAJI BORA, ALLIANCE ONE YAIBUKA KIDEDEA... - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 8 November 2024

MAKAMU WA RAIS AKABIDHI TUZO ZA MZALISHAJI BORA, ALLIANCE ONE YAIBUKA KIDEDEA...

 Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 

Makamu wa Rais Dk Isidory Mpango, amemwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye kukabidhi tuzo mzalishaji bora wa bidhaa za viwanda,huku kampuni ya tumbaku Alliance One,ikiibuka kidedea kwenye tuzo za Rais za Mzalishaji Bora(PMAYA) zinazoandaliwa kila mwaka na Shirikisho la viwanda nchini CTI.

Kampuni hiyo imekwapua ushindi huo kwenye eneo la wazalishaji wakubwa wa bidhaa za tumbaku,  ambapo kampuni zingine zaidi ya 42 zilichuana kwenye tuzo hizo za mwaka huu zilizofanyika Ijumaa Novemba 8.
Akiongea kwenye hafla hiyo Makamu wa Rais amewapongeza shirikisho la lenye viwanda nchini kwamba sekta hiyo ni nguzo muhimu kwenye uchumi wa taifa.

Amewapa changamoto tano ambazo amesema wazalishaji hao wanapaswa kuzifanyia kazi zikiwemo umuhimu wa kuvilea na kuvikuza viwanda vinavyochipukia ili viweze kukua zaidi na kuhimiri mtikisiko wa chumi za dunia.

Pia amesema wamiliki hao wa viwanda wanapaswa kuongeza nguvu kwenye utunzani wa mazingira pamoja na urejeshaji bidhaa viwandani yaani recycling kwa kiingereza.

Amewaasa wenye viwanda kuja na mkakati dhabiti utakaoweza kutoa ajira kwa vijana wengi wasio na ajira walioko mitaani,ambapo pia alisema serikali kwa upande wake imeanza kubadili aina ya elimu zinazotokewa nchini ili ziendane na fursa za ajira zilizopo mitaani.

Aidha amesema CTI wanapaswa kuja na mpango atazimi wa vijana ,lakini pia amewaasa wadau hao kujipanga ili kupambana na bidhaa feki zinazoingia kwa wingi nchini na kuharibu soko letu.

Msemaji wa Alliance One Wakili John Magoti amelishukuru shirikisho hilo kwa kutambua alama inayowekwa na kampuni hiyo kwenye sekta ya viwanda hususani vya kilimo.

Amesema tuzo ambayo wameipokea kwa miaka mitatu mfululizo unatokana ushirikiano mwema walionao kampuni hiyo na wafanyakazi na wadau wengine kwenye sekta ya tumbaku wakiwemo wakulima wanaofanya nao biashara.

Amesema kampuni yake imejipanga vizuri kuendelea kulichakata zao hilo hapa nchini ili sekta hiyo ndogo iendelee kushamiri na kuliingizia zaidi taifa pato la kigeni.

"Tumejipanga vizuri kuboresha zaidi utunzaji wa mazingira kiwandani na sasa tunaenda kutumia zaidi umeme jua wakati wa mchana na mpango huu tunauteleza kwa mahsusi kwani sekta yenu ni rafiki wa mazingira," amesema.

Naye Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe, amewapongeza CTI kwa kuziendeleza tuzo hizo walizozianzisha miaka 18 iliyopita,ambazo zimeleta ufanisi na ustawi wa uchumi wa nchi wa nchini.

"Serikali itaendelea kuweka na kutekeleza ya kuviendeleza viwanda vyetu nchini ambapo wakati huu tunarekebisha sera ya viwanda vikubwa na viwanda vidogo ili iweze kuwa na ufanisi zaidi,"amesema.

Aidha amesema serikali inaendelea kutenga maeneo ya ujenzi wa viwanda nchini,ambapo wilaya na mikoa yote imepokea maelekezo ya kufanya hivyo.

Amesema serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa viwanda ili kama nchiniweze kunufaika ujio wa eneo huru la Afrika ambalo limetarajiwa kuanza rasmi mwaka 2025.

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa shirikisho hilo Paul Makanza ameishukuru serikali sikivu ya Rais wa Jamhuri wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kusikia na kuondoa kero za wenye viwanda ambazo waliziwakilisha kwake mwaka jana.

Amezitaja kero hizo kuwa ni tatizo la umeme nchini,ambalo sasa limekwisha kabisa na nchi ina umeme wa ziada.

"Mwaka jana pia tulikuwa na tatizo la uhaba wa dola,ambalo limetatuliwa na mwaka huu halipo tena kwa maana halisikiki tena," amesema.

Ameishukuru serikali kuyapatia ufumbuzi matatizo ya kikodi miongoni mwa wanachama wa shirikisho hilo, ambapo pia serikali imeanzisha ofisi maalum ya kusikiliza kero za kitaifa za kikodi.

Pia ameiomba serikali kuangalia mbele na kushughulikia matatizo yanayojitokeza nchini ikiwemo uhaba wa shilingi pamoja na kucheleweshwa kwa malipo ya wakandarasi nchini.

Washindi wa jumla kwenye tuzo hizo ni Kampuni ya Sigara,TCC, wakifuatiwa Plascon ambao ameshika nafasi ya pili huku ALAF wakishika nafasi ya tatu.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe,(katikati) akimkabidhi Wakili John Magoti ambaye kampuni yake ya Alliance One imetwaa tuzo ya ushindi ya mzalishaji bora wa sekta ya bidhaa za tumbaku kwenye hafla ya utoaji tuzo hizo iliyofanyika leo Jiji Dar es Salaam.Anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa CTI Paul Makanza.Tukio hilo lilihudhuriwa pia Makamu wa Rais Isidor Mpango.






Wafanyakazi wa Alliance One wakifurahia tuzo yao.





No comments:

Post a Comment