DKT. NCHEMBA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA MAGEREZA CGP JEREMIA KATUNGU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 3 October 2024

DKT. NCHEMBA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA MAGEREZA CGP JEREMIA KATUNGU

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiagana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP Jeremiah Yoram Katungu, ambaye alifika ofisini kwake kujitambulisha na kuongelea mipango ya maendeleo ya Jeshi la Magerereza, katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP Jeremiah Yoram Katungu, akizungumza wakati wa kikao na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ambaye alifika ofisi za Hazina Jijini Dodoma kujitambulisha baada ya kuteuliwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuliongoza Jeshi la Magereza, hivi karibuni.

Kikao kikiendelea kati ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP Jeremiah Yoram Katungu, ambaye alifika Ofisi za Hazina Jijini Dodoma kujitambulisha baada ya kuteuliwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuliongoza Jeshi hilo, hivi karibuni.

Na Josephine Majura WF, Dodoma

WAZIRI wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP Jeremiah Yoram Katungu, ambaye amefika ofisini kwake kujitambulisha, akiwa ameambatana na Maafisa wengine wa ngazi ya juu wa Jeshi hilo, ambapo wamejadili masuala mtambuka ya namna ya kushirikiana ili kuhakikisha kuwa majukumu ya Jeshi hilo yanatekelezwa kwa ufanisi.

No comments:

Post a Comment