Naibu
Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya akisisitiza jambo alipokagua ukarabati
na ujenzi wa barabara ya Kilwa na Mkuranga-Kisiju Km 45 mkoani Pwani.
|
Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya akiwa wa wataalam katika ziara hiyo kukagua ukarabati na ujenzi wa barabara ya Kilwa na Mkuranga-Kisiju Km 45 mkoani Pwani. |
Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya akiwa katika ziara hiyo kukagua ukarabati na ujenzi wa barabara ya Kilwa na Mkuranga-Kisiju Km 45 mkoani Pwani. |
Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya akiwa katika ziara hiyo kukagua ukarabati na ujenzi wa barabara ya Kilwa na Mkuranga-Kisiju Km 45 mkoani Pwani. |
Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya akisisitiza jambo mara baada ya ziara yake kukagua ukarabati na ujenzi wa barabara ya Kilwa na Mkuranga-Kisiju Km 45 mkoani Pwani. |
Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya akisisitiza jambo alipokagua ukarabati na ujenzi wa barabara ya Kilwa na Mkuranga-Kisiju Km 45 mkoani Pwani. |
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya amezungumzia umuhimu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), kushirikiana na wananchi kulinda hifadhi za barabara na hivyo kuwezesha ujenzi wa miundombinu hiyo kufanyika kwa urahisi na kudumu kwa muda mrefu.
Akikagua ujenzi wa barabara ya Mkuranga - Kisiju KM 45
na barabara ya Kilwa mkoani Pwani amehimiza ushirikishwaji wa wananchi katika
kulinda hifadhi ya barabara ili kuepuka uvamizi wa hifadhi hizo hali
inayosababisha uchimbaji wa mchanga na mawe na hivyo kuathiri barabara na
madaraja wakati wa mvua.
"TANROADS waelimisheni wananchi ili wazuie wenzao
kulima, kujenga na kuchunga mifugo kwenye hifadhi za barabara ili kulinda
barabara na kuzikarabati kwa urahisi inapohitajika", ameelekeza Kasekenya.
Mkoa wa Pwani ni mkoa wa Viwanda hivyo ujenzi na ukarabati wa barabara hizi za Kilwa na
Mkuranga-Kisiju KM 45 uzingatie ubora na viwango vya juu ili kuwezesha magari
makubwa kusafirisha malighafi na bidhaa
za viwandani kwa urahisi wakati wote.
"Kukamilika kwa barabara ya Mkuranga -Kisiju
kutaongeza tija kwenye bandari ya kisiju na hivyo kuvutia wawekezaji wa Viwanda
na Hotel", amesisitiza Naibu Waziri Kasekenya.
Naibu Waziri Kasekenya amesema Serikali iko katika hatua
za mwisho kwa kushirikiana na Benki ya Dunia kufanya ukarabati mkubwa kwenye
maeneo yote ya barabara na madaraja yalioathiriwa pakubwa na mvua zilizonyesha
mwaka huu.
Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Pwani Eng. Zilli Kihoko
amesema watahakikisha hifadhi za barabara, maeneo ya maegesho na madaraja
yanalindwa ili yadumu na kuleta tija kwa wananchi.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA
MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA UJENZI.
No comments:
Post a Comment