Mtendaji Mkuu wa Benk ya I&M, Bw. Zahid Mustafa akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa huduma ya kisasa ya Rafiki Chat Bankin iliyoboreshwa inapatikana kupitia WhatsApp.
NA MUSSA KHALID
BENKI ya I&M imeanzisha huduma ya kisasa ya Rafiki Chat Bankin iliyoboreshwa ili kuwarahisishia huduma wateja wao.
Imeelezwa kuwa huduma hiyo ambayo inapatikana kupitia WhatsApp inatoa huduma mbalimbali za kibenki ikiwa ni pamoja na kuangalia salio la akaunti papo kwa papo, kupokea taarifa za miamala pamoja na kuhamisha au kutuma fedha kirahisi.
Akiuzungumza jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi huo Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Zahid Mustafa amesema benki hiyo inaendelea kufanya ubunifu kwa mustakabali endelevu na kuunga mkono ubadilishaji wa kigijitali nchini.
“Sisi kama I&M sio tu kwamba hii ni bidhaa yetu ya kwanza bali tupo tunajikita zaidi kwenye dhamira kuingia kwenye ulimwengu wa kidijitali lakini pia tumeingia ushirikiano na Airtel inaitwa kamilisha ambapo tunaweza kuwafikia watanzani wengi zaidi na kuwapa huduma bora zaid’amesema Mustafa
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha wateja Rejareja katika benki hiyo Simon Gachachi amesema kuwa malengo yao wanakusudia kuwekeza katika kujenga utendaji zaidi na vipengele vinavyofanya kazi kwa washirika wao wa teknolojia.
Aidha amesema kuwa katika huduma hiyo pia mwezi septemba watazindua namna mteja ataweza kulipa kodi na malipo mengine ya serikali kupitia WhatsApp kwa kutumia mifumo mbalimbali.
Amesema wameshirikiana serikali ambapo imechukua kipaumbele kusaidia benki kuendelea kufanya uwekezaji katika teknolojia ya ubunifu.
Akizungumzia huduma hiyo Meneja wa bidhaa za kidijitali wa benki hiyo Adam Emmanuel amesema kuwa huduma hiyo walianzisha tangu mwaka 2021 ambapo wamefanya maboreso mbalimbali ikiwemo kuwaruhusu wateja wapya kujisajili na kufungua akaunti.
Amesema kuwa vipengele vilivyoboreshwa ni pamoja na uwezo wa kujisajili mwenyewe unaotumia teknolojia ya AI,muonekano ulioboreshwa kwa mtumiaji,usaidizi wa wateja kwa msaada wa AI,na sehemu ya maswali na majibu yanayoulizwa mara kwa mara.
“Mchakato wa usajili ni rahisi tu ambapo ni sevu namba ya WhatsApp Banking iliyothibitishwa ya I&M Banki +255 755 674696 kisha tuma neon habari halafu fuata maelekezo’amesema Adam
Zainabu
Maalimu ni Mkuu wa Kitengo kwa wateja amesema hayo yote yanajiri kutokana na
kutimiza miaka 50 ya benki hiyo kwa mwaka huu hivyo wametambua muelekeo wa
dunia katika matumizi ya mitandao katika kufanya shughuli mbalimbali.
No comments:
Post a Comment