Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa kiwanda cha Sukari Mkulazi, Mbigiri mkoani Morogoro, tarehe 7 Agosti, 2024. |
Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Kasekenya akiwa na wataalam wake wakiangalia taswira na muonekaniko wa Kiwanda cha Sukari Mkulazi ambacho Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekizindua tarehe 7 Agosti, 2024. |
Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha Sukari Mkulazi, Mbigiri mkoani Morogoro, tarehe 7 Agosti, 2024. |
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi
Kiwanda cha Sukari Mkulazi kilichopo Mbigiri, Wilaya ya Kilosa Mkoa wa Morogoro
Agosti 7, 2024.
Kiwanda hiki kimeanza
uzalishaji wa sukari rasmi Julai 1, 2024 na kina uwezo wa kuzalisha Tani 50,000
za sukari kwa mwaka na kinazalisha Sukari ya Majumbani (Brown Sugar) na pia
kinatarajiwa kuzalisha Sukari ya Viwandani (Industrial Sugar) kwa mwaka
2024/2025
Kiwanda hiki
kinamilikiwa na Kampuni Hodhi ya Mkulazi ambayo Kampuni hii inamilikiwa kwa
ubia kati ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Shirika la Uzalishaji
Mali la Jeshi la Magereza (SHIMA).
No comments:
Post a Comment