Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa, Japhet Hasunga (Mb), (wa nne kushoto) wakikagua utekelezaji wa mradi wa ukarabati na uboreshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Tabora, Mkoani Tabora.
Kazi za ujenzi wa
jengo la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Tabora zikiendelea mkoani Tabora.
Jengo hilo litakapokamilika litaweza kuhudumia abiria 120 kwa wakati mmoja. |
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC)
imetembelea na kukagua mradi wa ukarabati na uboreshaji wa Kiwanja
cha ndege cha Tabora unaotekelezwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).
Kamati hiyo ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Mheshimiwa Japhet
Hasunga (Mb), ikiwa mkoani Tabora Machi 17, 2024 imeshauri kwa Wakala huo
masuala mbalimbali ikiwemo kumsimamia Mkandarasi kuongeza kasi ya utekelezaji
wa mradi huo ili wananchi wa Tabora na mikoa jirani waweze kunfaika na mradi
huo.
"Msimamieni Mkandarasi aongeze kasi ya utekezaji wa mradi ili ukamilike
kwa wakati, nao wananchi wa Tabora na mikoa jirani waweze kufurahia huduma ya
usafiri wa anga", amesema Hasunga.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Ludovick Nduhiye
amesema Wizara imepokea ushauri na maelekezo ya Kamati na kuahidi kuyafanyia
kazi kwa manufaa ya jamii na Taifa kwa ujumla.
Awali akiwasilisha taarifa ya mradi huo, Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi
Mohamed Besta amesema Mradi huo umefikia asilimia 38 na unahusisha Ujenzi wa
Jengo la abiria litakalohudumia abiria 120 kwa wakati mmoja, Mnara wa kuongoza
ndege, barabara ya kuingia na kutoka kiwanjani pamoja na ujenzi wa uzio wa
usalama wenye urefu wa kilometa 6.25
Mradi wa Uboreshaji na Ukarabati wa Kiwanja cha Ndege cha Tabora
utagharimu Tsh. Bil. 24 na unatarajiwa kukamilika tarehe 11 Oktoba 2024.

No comments:
Post a Comment