MAKAMU MWENYEKITI NEC AKAGUA MAANDALIZI YA UCHAGUZI MDOGO KATA YA KIMBIJI - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 13 March 2024

MAKAMU MWENYEKITI NEC AKAGUA MAANDALIZI YA UCHAGUZI MDOGO KATA YA KIMBIJI

 

Mawakala wa wagombea kutoka vyama mbalimbali vya siasa vilivyosimamisha wagombea katika uchaguzi wa udiwani Kata ya Kimbiji iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam wakila kiapo cha kutunza siri kwa mujibu wa sheria mbele ya Msimamizi Msaidizi wa Uchagazi ngazi ya Kata, Bw. Ricky Pascal, jana Machi 13,2024. Kimbiji ni miongoni mwa Kata 22 zinazotaraji kufanya uchaguzi mdogo wa madiwani Machi 20,2024. (Picha na NEC).

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk akiangalia orodha ya wagombea iliyobandikwa katika Kituo cha Kupigia Kura Shule ya Msingi Bohari iliyopo Kata ya Kimbiji katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam leo Machi 13, 2024. Jaji Mbarouk alitembelea vituo vya kupigia kura katika Kata ya Kimbiji kuangalia maandalizi ya Uchaguzi mdogo katika Kata hiyo inayotaraji kufanya uchaguzi Machi 20,2024 ambapo kata 22 zitafanya uchaguzi mdogo siku hiyo. Kulia ni Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kigamboni, Bw. Erasto Kiwale. (Picha na NEC).


No comments:

Post a Comment