BILIONI 101.2 KUJENGA BARABARA YA KAHAMA-KAKOLA KM 73 KWA KIWANGO CHA LAMI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday 18 March 2024

BILIONI 101.2 KUJENGA BARABARA YA KAHAMA-KAKOLA KM 73 KWA KIWANGO CHA LAMI

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa (Mb) akishuhudia utiaji saini mkataba wa ujenzi wa barabara ya Kahama - Bulyanhulu Jct – Kakola (KM 73) kwa kiwango cha lami kati ya Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mha. Mohamed Besta na Meneja wa Mradi kutoka Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC), Bw. Liu, leo tarehe 16 Machi 2024 katika Uwanja wa Shule ya Msingi ya Kakola Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara (TANROADS), Mha. Mohamed Besta na Meneja wa Mradi kutoka Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC), Bw. Liu wakionesha Mkataba wa ujenzi wa barabara ya Kahama - Bulyanhulu Jct – Kakola (KM 73) kwa kiwango cha lami mara baada ya kutiliana saini mbele ya Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa (Mb), leo tarehe 16 Machi, 2024 katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kakola Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.

Serikali imesaini Mkataba wa ujenzi wa barabara ya Kahama-Bulyanhulu Jct - Kakola (km 73) kwa kiwango cha lami ili kufungua fursa za kiuchumi za madini, Kilimo, Misitu na Utalii katika mikoa ya Shinyanga, Geita, Tabora, Kagera na Kigoma.

Mkataba huo umesainiwa kati ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation kwa gharama ya Shilingi Bilioni 101.2 kwa ufadhili wa Kampuni ya Madini ya Barrick Tanzania Mining Companies (BTMCs) na Serikali ya Tanzania.

Akishuhudia Utiaji Saini wa barabara hiyo Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa barabara hii imekuwa ni kilio cha muda mrefu na sasa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ushirikiano mzuri na wawekezaji wa ndani ya nchi ikiwemo kampuni ya Barick ametoa kibali barabara hiyo iweze kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami.

“Niwashukuru Barrick kwa ushirikiano ambao mmetupa kwa ujenzi wa hizi kilometa 73 na kwa hilo niwahakikishie wananchi tumewaletea Mkandarasi ambaye ni mbobezi na mwenye uwezo mkubwa na kwa namna tulivyojipanga na usimamizi makini nitakaouweka kwenye hii barabara msiwe na wasiwasi tutatimiza utekelezaji wake ndani ya miezi 27 na si zaidi ya hapo”, amesema Bashungwa

Aidha, Bashungwa ameeleza kuwa Mhe. Rais pia ameelekeza Wizara ya Ujenzi kuanza hatua za kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Iloginhadi Mtakuja (km 57.4) ambayo ni barabara ya kiuchumi na inaunganisha Mkoa wa Shinyanga na Geita.

Bashungwa amemuagiza Mtendaji Mkuu wa TANROADS   kwa kushirikiana na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Mijini na Mijini (TARURA) kuona namna ya kuboresha miundombinu ya barabara za Mji wa Kahama ili kuusaidia mji huo katika ukuaji wake wa Kiuchumi na kijamii.

Aidha, Bashungwa amewahakikishia wananchi kuwa mtandao wa barabara kwa zile za changarawe na zile za lami zilizopo Mkoani Shinyanga zitaendelea  kusimamiwa na kuhudumiwa ili ziweze kupitika msimu wa kiangazi na vuli ikiwemo barabara ya Old Shinyanga - Solwa - Burige mpaka Kahama pamoja na ile Kolandoto-Lalago.

Bashungwa amemtaka Mkandarasi huyo kuona namna ya kuchangia huduma za kijamii kwa wananchi wanaouzunguka mradi huo pamoja na kushirikiana na wananchi wakati wa utekelezaji wa mradi.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Eng. Mohamed Besta ameeleza kuwa 

No comments:

Post a Comment