![]() |
Waziri wa Ujenzi
akisisitiza jambo kwa Menejimenti na Mameneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme
(TEMESA), kutoka Mikoa yote nchini (hawapo pichani), wakati wa Wasilisho la
Maboresho na Mikakati ya Kujitangaza ya Wakala huo, jijini Dodoma. Kushoto
kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Eng. Aisha Amour na Kulia ni Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ludovick Nduhiye.
Bashungwa amezungumza
hayo jijini Dodoma Februari 5, 2024 mara baada ya kupokea wasilisho la Wakala
huo ambao unaelezea mkakati wa kujitangaza na kupata mwarobaini wa changamoto
mbalimbali ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na Wateja kwa Wakala huo.
"Nimefurahishwa
na mkakati huu mliouandaa, ni matumaini yangu TEMESA sasa mtabadilika na
mtafanya maboresho makubwa katika utoaji wenu wa huduma kama mlivyoeleza",
amesema Bashungwa.
Bashungwa ametaka Wakala
huo kujikita katika hudoaji wa huduma kwa Watanzania na kuondokana na dhana ya
kuweka tozo kubwa ambayo itamnyonya mwananchi kwenye huduma wanazozitoa.
Aidha, Bashungwa
ameagiza Wakala huo kukaa mezani na kampuni ya TOYOTA ili kufikia muafaka wa
makubaliano ya ununuzi wa vipuri, kubadilishana utaalam na utoaji wa mafunzo
kwa wataalam wa TEMESA.
Bashungwa ameeleza
kuwa Chimbuko la Mkakati huo limetokana na malalamiko ya wateja kwa TEMESA
ikiwemo kutoridhishwa na huduma za Wakala huo katika karakana za Wakala huo
ikiwemo uwepo wa vipuri feki, wizi wa vipuri na
kuchelewesha huduma kwa wateja wao.
Kadhalika, Bashungwa
amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Mhandisi Aisha Amour,
kuisimamia Timu ya Mkakati wa TEMESA ili kuhakikisha mafunzo kwa mafundi
yanapatikana, upatikanaji na uwepo wa vipuri halisi, uwepo wa Software mbalimbali ambazo zinamilikiwa
na Serikali, uwepo wa muongozo wa ramani za majengo ya abiria katika vituo
vyote nchini pamoja na uwepo wa muongozo wa kutumia ramani moja katika karakana
zote nchini.
Kwa upande wake,
Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Lazaro Kilahala, amesema kuwa lengo la kuandaa mkakati
huo ni kuendelea kuboresha Wakala huo kupitia huduma zake ambazo unazitoa kwa
wateja wake.
Kilahala ametaja mapendekezo yaliyomo kwenye mkakati huo ni pamoja na uboreshaji wa maaeneo ya maegesho ya abiria, kuwa na mitambo imara na kuwa na sehemu ya kupumzikia wateja katika karakana wakati wakisubiri hudum


No comments:
Post a Comment