USHIRIKISHWAJI VIKUNDI VYA KIJAMII KWENYE MATENGENEZO YA BARABARA 'WAMKOSHA' MHANDISI SEFF - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday 6 January 2024

USHIRIKISHWAJI VIKUNDI VYA KIJAMII KWENYE MATENGENEZO YA BARABARA 'WAMKOSHA' MHANDISI SEFF


USHIRIKISHWAJI vikundi vya kijamii kwenye matengenezo ya barabara ya Kisangara kwenda Shighatini wilayani Mwanga umemfurahisha Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff.

Mhandisi Seff amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya hiyo kukagua mradi wa matengenezo katika barabara hiyo yenye urefu wa Km. 25, unaofanywa na kikundi maalum cha kijamii kiitwacho Muhako Engineering, kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro.

Mhandisi Seff amesema amefurahishwa sana na ushirikishwaji huo wa vikundi vya kijamii katika utekelezaji wa miradi katika matengenezo ya barabara kwani jamii inayozunguka miradi hiyo inapata ajira na kuweza kuinuka kiuchumi.

Ametumia ziara hiyo, kutoa wito kwa Halmashauri kuwajengea uwezo na kuhamasisha vikundi vya kijamii ili viweze kufanya kazi za matengenezo ya barabara ili kufikia asilimia 30 ya bajeti zinazotengwa  kwa ajili ya  kazi  hizo kila mwaka ambapo kunawawezesha kuinuka kiuchumi na kuondokana na umasikini.

Naye Mkurugenzi wa ufundi wa Kikundi cha Muhako Engineering Bw. Stephen Mkeni alimueleza Mtendaji Mkuu kwamba wananchi katika eneo la mradi wameshirikishwa vyema kwenye kazi zinazoendelea na hivyo wameweza kupata ajira na kuwawezesha kujikimu kimaisha pamoja na familia zao.

Wakala ya barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) hushirikisha vikundi maalum katika shughuli mbalimbali za matengenezo ya barabara ili kuwezesha jamii kukuza uchumi wao binafsi pia kuhakikisha wanatunza miundombinu inayozunguka maeneo yao.

No comments:

Post a Comment