TMA YATOA RASMI UTABIRI WA MVUA MAENEO YANAYOPATA MSIMU MMOJA KWA MWAKA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday 31 October 2023

TMA YATOA RASMI UTABIRI WA MVUA MAENEO YANAYOPATA MSIMU MMOJA KWA MWAKA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Makamu Mwenyekiti Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia Nchi (IPCC), Dkt. Ladislaus Chang’a, akizungumza wakati wa mkutano na vyombo vya habari akitoa mwelekeo wa mvua za Msimu, katika ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam,Tarehe 31 Oktoba, 2023. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Kulia ni Kaimu Meneja Kituo Kikuu cha Utabiri, Dkt. Alffred Kondowe

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Ladislaus Chang’a, akizungumza wakati wa mkutano na vyombo vya habari akitoa mwelekeo wa mvua za Msimu, katika ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa TMA, Dk. Hamza Kabelwa pamoja na Kaimu Meneja Kituo Kikuu cha Utabiri, Dkt. Alffred Kondowe wakifuatilia (kulia)

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Ladislaus Chang’a, akifafanua jambo wakati wa mkutano na vyombo vya habari akitoa mwelekeo wa mvua za Msimu, katika ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa TMA, Dk. Hamza Kabelwa akifuatilia.

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa rasmi mwelekeo wa mvua za Msimu kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka ambayo ni mikoa ya  Tabora, Katavi, Kigoma, Singida, Dodoma, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe, Lindi, Mtwara, Ruvuma na  na Kusini mwa Morogoro. 

Taarifa hiyo imesema  kipindi cha nusu ya msimu (Novemba 2023 hadi Januari, 2024) kinatarajiwa kuwa na mvua nyingi ukilinganisha na nusu ya pili (Februari hadi Aprili 2024), uwepo wa El-Niño unatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika mvua za Msimu.

“Mvua za Juu ya Wastani hadi Wastani zinatarajiwa katika maeneo ya kusini mwa mkoa wa Morogoro, mikoa ya Iringa, Lindi, Mtwara, Singida, Dodoma, kaskazini mwa mkoa wa Katavi, Kigoma na Tabora. Aidha, mvua za Wastani hadi Juu ya Wastani zinatarajiwa kusini mwa mkoa wa Katavi, mikoa ya Njombe, Rukwa, Songwe, Mbeya na Ruvuma”. Alisema Dkt. Ladislaus Chang’a, 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu TMA na Makamu Mwenyekiti Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia Nchi (IPCC) wakati wa mkutano na vyombo vya habari kuhusiana na mwelekeo wa mvua za Msimu, katika ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam,Tarehe 31 Oktoba, 2023. 

No comments:

Post a Comment