NAIBU WAZIRI KIHENZILE APIGILIA MSUMARI STAHILI ZA VIBARUA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 6 October 2023

NAIBU WAZIRI KIHENZILE APIGILIA MSUMARI STAHILI ZA VIBARUA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Ladislaus Chang'a akiwatambulisha viongozi mbalimbli wa TMA kwenye ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile alipotembelea Ujenzi wa Jengo la Kituo Kikuu cha Hali ya Hewa linalojengwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA).

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile akitoa maelekezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dkt. Burhan Nyenzi alipafanya ziara kukagua ujenzi wa Jengo la Kituo Kikuu cha Hali ya Hewa linalojengwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA).

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile (wa kwanza kulia) akikagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Kituo Kikuu cha Hali ya Hewa linalojengwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Ladislaus Chang'a (kulia) akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile (kushoto) alipotembelea Ujenzi wa Jengo la Kituo Kikuu cha Hali ya Hewa linalojengwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA).

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile (kushoto) akitoa maelekezo mara baada ya ziara yake kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Kituo Kikuu cha Hali ya Hewa linalojengwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA).

Muonekano wa Ujenzi wa Jengo la Kituo Kikuu cha Hali ya Hewa linalojengwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA).

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Ladislaus Chang'a akizungumza kumkaribisha Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile alipofanya ziara kukaguia maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Kituo Kikuu cha Hali ya Hewa linalojengwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA).

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile (kulia) akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Ladislaus Chang'a mara baada ya ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Kituo Kikuu cha Hali ya Hewa linalojengwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA).

NAIBU Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile ameitaka Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) kuhakikisha vibarua wote wanaofanya kazi katika Ujenzi wa Jengo la Kituo Kikuu cha Hali ya Hewa kuhakikisha wanapata stahili zao kwa wakati ili kutokwamisha mradi huo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mara baada ya kukagua mradi huo Naibu Waziri Kihenzile amesema kunyimwa haki kwa vibarua imekuwa ni moja ya sababu zinavyogombanisha wananchi na Serikali na kukwamisha miradi kukamilika kwa wakati.


“Miradi mingi inayotekelezwa nchini hususani kwenye Uchukuzi kumekuwa na malalamiko ya kutolipewa kwa vibarua na Mkandarasi anakuwa ameshalipwa sasa kasimamieni eneo hilo na muhakikishe mnaisimamia kampuni inayojengwa ili haya yasiendelee kutokea’ amesema Naibu Waziri Kihenzile.


Naibu Waziri Kihenzile ameipongeza TMA kwa kuendelea kutoa taarifa za hali ya hewa kwa wakati hali inayosaidia wakulima na wadau wote kupata taarifa sahihi kwa utekelezaji wa miradi na kilimo.


Aidha, Naibu Waziri Kihenzile ameitaka TMA kuongeza mbinu za utoaji wa elimu ili kuhakikisha kila mdau anafikiwa kwa wakati na kwa taarifa sahihi za hali ya hewa.


Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dkt. Burhan Nyenzi amesema TMA itaendelea kuhakikisha wananchi wote wanafikiwa ili kuwarahisishia shughuli za ujenzi na kilimo.


Kwa upande Wake Mshauri Mwelekezi Kutoka Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT) John Malisa amemuhakikishia Naibu Waziri wa Uchukuzi Kihenzile kuwa mradi unakwenda vizuri pamoja na changamoto za mvua zilizoanza kunyesha utakamilika kwa wakati.


Mradi wa ujenzi wa jengo Kituo cha Hali ya Hali ya Hewa kinachojengwa jijini Dar es Salaam kitagharimu takribani bilioni 9 na unatarajiwa kukamilika Julai mwakani.


(Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Uchukuzi)

No comments:

Post a Comment