WALIMU MAKADA CCM KANDA YA ZIWA WAENZI MUUNGANO KWA KUFIKA KIZIMKAZI ZANZIBAR - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 28 September 2023

WALIMU MAKADA CCM KANDA YA ZIWA WAENZI MUUNGANO KWA KUFIKA KIZIMKAZI ZANZIBAR

Walimu makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika picha ya pamoja mbela ya Ofisi ya chama hicho Tawi la Kizimkazi Mkunguni baada ya kuwasili katika Sheia hiyo.

Mlezi na Mraribu wa ziara ya walimu Makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Richard Bundala (Kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ayub Mohamed Mahmoud (kulia) katika Hotel ya Riu baada ya kupata chakula cha mchana na walimu hao.

KATIKA kudumisha muungano wa Tanzania Bara na Tanzania visiwani, Shirikisho la walimu  makada wa chama cha mapinduzi - CCM, Kanda ya Ziwa,  Wamefanya ziara katika kisiwa cha Zanzibar pamoja na kutembelea Sheia ya kizimkazi alipozaliwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Walimu hao takribani 50  kutoka mikoa sita ya kanda hiyo wamewasili  kisiwani Zanzibar, kwa lengo la kudumisha muungano wa Tanzania bara na Tanzania Visiwani pamoja na kufanya utalii wa ndani.


Miongoni mwa maeneo waliofika ni katika Sheia ya Kizimkazi, mahali ambapo ni chimbuko la Rias Samia Suluhu Hassan, ambapo wamepokelewa katika ofisi ya chama cha mapinduzi CCM Tawi la Kizimkazi Mkunguni.


Akizungumza katika ofisi hiyo mlezi na mratibu wa shirikisho la walimu makada wa chama cha mapinduzi CCM Bundala Richard amesema wamefika Kizimkazi kudumisha Muungano pamoja na kuona mahali ambapo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan alizaliwa, ikiwani kuenzi na kueshimu kile anachokifanya kwa watanzania kwa kuleta maendeleo kwenye.


“Walimu kufika hapa Kizimkazi,kwanza itasaidia kuendelea kuuenzi na kudumisha Muungano wetu kwani Mwalimu akijua umuhimu wa Muungano wanafunzi wataambukizwa kile ambacho Mwalimu amejifunza kwa Kuja huku  Kisiwani Zanzibar,”Amesema Bundala 


Aidha amesema Walimu makada wa chama cha mapinduzi ni chachu katika kueneza mazuri yanayofanya na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuleta maendeleo ya taifa kutokana na walimu hao kuwa karibu na jamii.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa shirikisho hilo la Walimu Makada wa chama Cha mapinduzi - CCM Jackson Kaduti amewashukuru Wazanzibar kwa Kuwazaliwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutokana na kuleta maendeleo kwenye taifa bila kujadili ukanda, ukabila wala Unzanzibar na Ubara. Amesema.


“Mimi Nina muda mrefu kidogo nikiwa mwalimu,kwa maboresho ya elimu na miundombinu ya madarasa yanayojengwa na rais Samia sijawahi kuona katika utumishi wangu wote, shule zingine tumeipa Majina yake kwa mfano Chif Hangaya”. 


Mkuu wa mkoa wa kaskazini Unguja Ayub Mohamed Mahmoud amekuwa mwenyeji wa Walimu hao ambapo amesema kuenzi Muungano wa Tanzania bara na Zanzibar ni silaha muhimu katika kudumisha amani na mshikamano miongoni mwa Tanzania, ambapo pia ameeleza vivutio vya utalii vilivyopo katika kisiwa hicho. Ayoub amesema.


 “Mwaka jana tulifanya tathimini ya vivutio Vya utalii vilivyopo katika mkoa wetu, Tumebaini zaidi ya vivutio vya utalii  415”


Baadhi ya walimu walioshiriki katika ziara hiyo akiwemo Katibu wa shirikisho hilo David Sulube na Mwalimu Vivian Nyambui, wamesema Ziara hiyo inawajenga kiakili na kimwili ambapo pia itawasaidia kueneza kwa wanafunzi Umuhimu wa kudumisha Muungano.


Shirikisho hilo la walimu makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka mikoa ya kanda ya ziwa wanatoka katika mikoa sita ya kanda hiyo ikiwemo Mwanza, Mara, Simuyu, Shinyanga, Geita na Kagera.


No comments:

Post a Comment