BILLIONI 18.5 KUWEZESHA WANAFANYABIASHARA NDOGO NDOGO KIUCHUMI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday 16 September 2023

BILLIONI 18.5 KUWEZESHA WANAFANYABIASHARA NDOGO NDOGO KIUCHUMI

Naibu Waziri wa Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe Mwanaidi Ali Khamis akikagua ujenzi wa mabweni katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Misungwi wakati wa ziara yake mkoani Mwanza Septemba 15, 2023.

KATIKA kuwawezesha wajasirimali wadogo wadogo hasa wanawake Serikali imetengwa jumla ya Shillingi 18.5 kwaajili ya kuwasaidia kupata mikopo yenye riba nafuu.

Hayo yamesemwa Septemba 15, 2023 na Naibu Waziri wa Jamii ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe Mwanaidi Ali Khamis alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Mondo wakati wa ziara yake Wilayani Misungwi Mkoa Mwanza.

Naibu Waziri Mwanaidi amesema lengo la Serikali ni kuwasaidia wananchi katika kujikwamua kiuchumi hivyo utoaji wa mikopo hiyo itasaidia wajasirimali wadogo wadogo hasa Wanawake kupata mitaji itakayowawezesha kuboresha biashara zao.

Aidha amekipongeza Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Misungwi kwa ubunifu wa utengezaji wa mitungi ya maji kwa kutumia saruji ili kuvuna maji ya mvua na kuondokana na changamoto za upatikanaji wa maji katika jamii.

"Hongera sana Mkuu wa Chuo jambo hili ni la kuigwa kwani umeshusha utaalam wa Maendeleo ya Jamii na ufundi kwa wananchi ili waweze kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili" alisema Naibu Waziri Mwanaidi.

Pia Naibu Waziri Mwanaidi amewamasisha Wanawake na Jamii kwaujumla kushirikiana kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto katika jamii hasa kuzingatia Malezi na Makuzi ya Mtoto na kulinda utamaduni wa mtanzania.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Paulo Chacha amesema Wilaya hiyo inaendelea na juhudi mbalimbali za kuhamasisha wananchi kujitolea katika shughuli za maendeleo, ujenzi wa Makazi bora na kupambana na vitendo vya ukatili hasa ndoa za utotoni katika jamii.

"Mhe. Naibu Waziri huku kwetu wananchi wanahamasikia sana katika shughuli za maendeleo pia katika kuboresha Makazi kama ulivyojionea mwenyewe lakini tunapambana na vitendo vya ukatili hasa kwa kushirikiana na vikundi mbalimbali hasa vya Wanawake" alisema Chacha.

Akisoma taarifa ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Misungwi Mkuu wa hicho Charles Achioga amesema Chuo kinashirikiana na jamii ya Wilaya ya Misungwi katika kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia, ari ya kujitolea katika shughuli za maendeleo na kuibua na kutekeleza miradi mbalimbali katika jamii kwa kutumia wanafunzi wanaosoma na waliohitimu katika Chuo hicho.

Wakati huo huo Naibu Waziri Mwanaidi ametembelea na kukagua ujenzi wa mabweni ya ghorofa mbili lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 352 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Misungwi linalogharimu shillingi 300 na litatatua changamoto za uhaba wa mabweni kwa watoto wa kike Chuoni hapo.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe Mwanaidi Ali Khamis yupo katika ziara ya kikazi kwa Mikoa ya Kanda ya Ziwa kufuatilia utekelezaji wa Sera Mipango na afua mbalimbali za maendeleo na Ustawi wa Jamii nchini.

No comments:

Post a Comment