Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo aliyesimama mwenye shati jeupe akimtambulisha mkandarasi wa mradi wa maji wa tarafa ya Naipanga Shaban Kimaro kutoka kampuni ya Broadway Engineering co.LTD wenye gharama ya zaidi ya bilioni 1.18 Kwa lengo la kutatua kero ya maji kwa kumtua mama ndoo kichwani.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Adinani Mpyagila akimshukuru Rais Dr Samia suluhu Hassan kwa kutatua kero ya maji katika Tarafa ya Naipanga.
Meneja wa RUWASA wilaya ya Nachingwea Mhandisi Sultan Ndolwa akielezea namna ambavyo mradi huo utatekelezwa na kutatua kero ya maji kwa wananchi wa Tarafa ya Naipanga.
Na Fredy Mgunda, Nachingwea
BAADA ya kilio cha miaka mingi cha wananchi wa Tarafa ya Naipanga wilayani Nachingwea kwa kukosa maji hatimaye Serikali ya awamu ya sita imepeleka mradi wa zaidi ya bilioni 1.18 kutatua kero hiyo ya maji.
Akizungumza wakati wa kumtambulisha mkandarasi wa mradi huo, Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa alisikiliza kero za wananchi kuhusu tatizo la maji na hatimaye Serikali imeifanyia kazi.
Moyo alisema kuwa mradi huo utahusisha kata za Naipanga, Chiumbati, Rahaleo na Stesheni ambazo zitanufaika Moja kwa Moja na mradi utahudumia vijiji 11 na wananchi 19,110 lengo likiwa kuwatua ndoo akina mama wa Tarafa ya Naipanga.
Alisema kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dr Samia suluhu Hassan imekuwa sikivu kutatua kero za wananchi ndio maana hata mradi huo imekuwa rahisi kuupata.
Moyo aliwaomba wananchi kuchangamkia fursa mbalimbali zitakazojitokeza wakati wa mradi huo ukiwa unatekelezwa huku akiwataka kuacha tabia ya kuwaibia vifaa wakandarasi wanavyotekeleza mradi huo.
Kwa upande wa meneja wa RUWASA wilaya ya Nachingwea mhandisi Sultan Ndolwa alisema kuwa mradi utakuwa na tenki Moja lenye ujazi wa Lita za maji 300,000,uzio, vituo 40 vya kuchotea maji vyenye sehemu 2 Kila kimoja na mtandao wa mabomba wenye urefu wa kilometa 32,425.
Mhandisi Ndolwa alisema kuwa mradi huo utakamilika baada ya miezi kumi na mbili Kwa mujibu wa mkataba aliosaini mkandarasi wa mradi huyo Broadway engineering Co LTD na mradi huo unajengwa chini ya mpango wa lipa Kwa matokeo na kusimamiwa na wakala wa usafi wa mazingira vijijini (RUWASA).
Naye mkurugenzi wa Broadways Engineering co. Ltd Shaban Kimaro alisema kuwa atakamikisha mradi Kwa wakati ili kuwatua ndoo kichwani wanawake kama ambavyo dhamira ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dr Samia suluhu Hassan inavyotaka.
Kimaro alisema kuwa anaomba ushirikiano na wananchi wa vijiji vyote vya Tarafa ya Naipanga katika kipindi chote ambacho mradi unatekelezwa.
No comments:
Post a Comment