UWANJA WA KWARAA KUTUMIKA KILELE CHA MWENGE WA UHURU - NAIBU WAZIRI KATAMBI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday 12 August 2023

UWANJA WA KWARAA KUTUMIKA KILELE CHA MWENGE WA UHURU - NAIBU WAZIRI KATAMBI

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi akikagua ujenzi wa uwanja wa Kwaraa akiwa ameambatana na Viongozi wa Mkoa wa Manyara pamoja wajumbe wa kamati ya maandalizi ya wakati  wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya uwanja huo tarehe 11 Agosti 2023 kuelekea kilele cha mbio hizo Mkoani Manyara.

Mkandarasi wa Uwanja huo, Mhandisi Theophan Rantaley (wa tatu kutoka kulia) akitoa taarifa ya hatua zilizofikiwa ujenzi wa Majukwaa wakati wa ziara ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi (wa pili kutoka kulia) alipotembelea uwanja huo Agosti 11, 2023 Mkoani Manyara.

Na Mwandishi Wetu - MANYARA

NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi amemuagiza mkandarasi anayejenga uwanja wa mpira wa Kwaraa kumaliza kwa wakati ili kutumika katika kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru.

 

Mhe. Katambi ametoa maelekezo hayo  Agosti 11,2023 wakati  wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya uwanja huo kuelekea kilele cha mbio hizo  za  zitakazohitimishwa Oktoba 14, 2023.

 

Aidha, amesema kuwa ujenzi wa uwanja huo ni mpango wa Serikali katika kuwasongezea karibu viwanja vya michezo wananchi wa Mkoa wa Manyara lakini pia utakautumika kwenye kilele hicho.

 

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Babati, Mhe. Lazaro Twange amemhakikishia Naibu Waziri kuwa kuwa watamsimamia mkandarasi ili ujenzi huo ukamilike ndani ya muda uliopangwa.

 

Katika ziara hiyo, Mhe. Katambi amekagua  pia Kanisa Katoliki Parokia ya Roho Mtakatifu Ngarenaro -Manyara itakapo fanyika ibada ya Baba wa Taifa, uwanja wa stendi ya zamani itakapofanyika wiki ya vijana na kukagua maendeleo ya vijana wa halaiki katika Shule ya Sekondari ya kutwa ya Babati.

No comments:

Post a Comment