MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila Agosti 15, 2023 amekagua na kuongea wafanyabishara wa samaki katika Soko la Ferry Ilala -Jijini Dar es Salaam.
RC Chalamila akiongea na wafanyabishara hao amesema Mhe Rais Dkt Samia anania njema na wafanyabishara katika soko hilo ambapo amewataka kila mmoja anayefanya biashara katika Soko hilo kuwa mlinzi wa mwenzie ili idadi ya wafanyabishara iliyopo sasa ya zaidi 3,000 isiongezeke hadi pale Serikali itakapofanya maboresho ya Soko.
Aidha RC Chalamila amesema ujio wake katika soko hilo amebaini uholela wa Wafanyabishara, kukosekana kwa uaminifu miongoni mwa wafanyabishara kupitia kiwango cha mapato ambacho kinatakiwa kipatikane, ubovu wa miundombinu, sheria sio shirikishi hivyo ni wakati muafaka wa kuanza kupangana, pia Meneja kuwa na ubunifu zaidi katika kuongeza mapato vilevile kupitia sheria zilizoko kwa kuwa shirikisha wafanyabishara wenyewe.
Hata hivyo RC Chalamila ameagiza kupunguza matumizi ya mkaa katika soko hilo ambayo huzalisha moshi ambapo amewataka kuanza matumizi ya gesi
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya IIala Mhe Edward mpogolo akiongea kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa amesema pamoja juhudi kubwa inayofanywa na Wilaya hiyo ziko Changamoto kadhaa katika soko hilo ikiwemo migogoro kati ya zone moja na nyingine, Ukosefu wa friji la kuifadhia samaki kwa baadhi ya maeneo, wafanyabishara ni zaidi ya elfu 3, na kuwepo kwa mchanga kando ya ferry hiyo ambapo awali meli za samaki zilikuwa zinatia nanga na siku hizi haiwezekani hivyo ujio wa Mhe Mkuu wa Mkoa imekuwa faraja kubwa na wako tayari kumsikiliza na kupokea maagizo na maelekezo yake kwa masilahi mapana ya wafanyabishara katika soko hilo.
No comments:
Post a Comment