KAMATI YA BUNGE YAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA UWEZESHAJI VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday 15 August 2023

KAMATI YA BUNGE YAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA UWEZESHAJI VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana pamoja na Programu ya Taifa ya Ukuzaji Ujuzi kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii tarehe 15 Agosti, 2023 Bungeni jijini Dodoma.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii wakifuatilia wasilisho la Utekelezaji wa Programu ya Taifa ya Ukuzaji Ujuzi wakati wa kikao hicho.

Na Mwandishi Wetu – DODOMA

KAMATI ya Bunge ya Ustawi wa Maendeleo ya Jamii imempongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha ustawi wa vijana na Watu wenye Ulemavu kujikwamua  kiuchumi.

 

Kauli hiyo imetolewa Agosti 15, 2023 bungeni na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Fatuma Toufiq kwenye kikao cha kamati cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana pamoja na utekelezaji wa Programu ya Taifa ya Ukuzaji Ujuzi inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

 

Aidha, Mhe. Fatuma Toufiq amesema kamati hiyo itaendelea kuishauri Serikali kuendelea kuongeza wigo wa kuwezesha vijana wengi zaidi kupata mikopo, fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali.

 

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako ameeleza kuwa Ofisi yake imefanya maboresho ya mwongozo wa mfuko huo mwaka 2023 ili kupanua wigo wa viwango vya mkopo inayotolewa sambamba na kumwezesha mtu moja moja kukopa badala ya kikundi.

 

Naye, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Prof. Jamal Katundu amesema kuwa, ofisi hiyo imetenga Sh.Bilioni moja katika mfuko wa Watu wenye Ulemavu kwa ajili ya utekelezaji wa afua mbalimbali za kundi hilo.

No comments:

Post a Comment