RAIS SAMIA AFUNGUA JENGO LA KITEGA UCHUMI (SAFINA HOUSE) LA KANISA ANGLIKANA TANZANIA, JIJINI DODOMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 14 August 2023

RAIS SAMIA AFUNGUA JENGO LA KITEGA UCHUMI (SAFINA HOUSE) LA KANISA ANGLIKANA TANZANIA, JIJINI DODOMA

 

Muonekano wa Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa la Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Central Tanganyika ambalo limefunguliwa Rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu tarehe 15 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Maaskofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania wakati akikata utepe kuashiria ufunguzi Rasmi wa Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa hilo kwenye Sherehe zilizofanyika katika viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta utepe pamoja na Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) Dkt. Dickson Chilongani kuashiria ufunguzi Rasmi wa Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa hilo kwenye Sherehe zilizofanyika katika viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2023. Engine katika picha ni Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Mhashamu Dkt. Maimbo Mndolwa pamoja na Maaskofu wengine wa Kanisa hilo nchini.

No comments:

Post a Comment