KATIBU MKUU YAKUBU AHIMIZA VYAMA NA MASHIRIKISHO YA MICHEZO KUJIUNGA NA VYAMA VYA MICHEZO HUSIKA AFRIKA NA DUNIA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday 24 July 2023

KATIBU MKUU YAKUBU AHIMIZA VYAMA NA MASHIRIKISHO YA MICHEZO KUJIUNGA NA VYAMA VYA MICHEZO HUSIKA AFRIKA NA DUNIA

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Chama cha Mchezo wa Kabaddi mara baada ya kikao kilichofanyika Julai 24, 2023 jijini Dar es salaam. Na wa nne kulia ni Mwenyekiti wa Mchezo wa Kabaddi Tanzania Abdallah Nyoni.

Na Eleuteri Mangi, Dar es Salaam

KATIBU Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amekutana na kufanya vikao na baadhi ya Vyama na mashirikisho ya Sanaa na Michezo ambapo amewahimiza kujiunga na vyama au mashirikisho ya vya vyama hivyo Afrika na Dunia.

 

Vikao hivyo vimefanyika Julai 24, 2023 jijini Dar es salaam kwa nyakati tofauti tofauti ambapo alikutana na Chama cha Mchezo wa Kabaddi, Uongozi wa Mchezo wa Wanyanyua Vitu Vizito, Mchezo wa Ngumi za Ridhaa, uongozi wa Shirikisho la Mchezo wa Mieleka pamoja na Uongozi wa Kituo cha Sanaa na Utamaduni kwa Viziwi Tanzania (KISUVITA).

 

Katika vikao hivyo wamejadili mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta za Sanaa na Michezo nchi ili kuleta tija kwa wasanii na wanamichezo nchini.

 

Kwa upande wa Serikali wameongozwa na Katibu Mkuu Bw. Saidi Yakubu, Dkt. Emmanuel Ishengoma, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa, Bw. Alli Mayayi, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Dkt. Kedmon Mapana, Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bi Neema Msitha, Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa (BMT) wakati kwa upande wa wadau alioshiriki ni Abdallah Nyoni, Mwenyekiti wa Mchezo wa Kabaddi Tanzania, Bw. Andrew Kapeleka, rais wa Shirikisho la Mchezo wa Mieleka Tanzania, Bw. Habibu Mrope Mkuu wa Kituo cha Utamaduni na Sanaa Tanzania kwa Viziwi Tanzania (KISUVITA), Lorraine D'arcy kutoka Australia pamoja na Bw. Lukelo Wililo, rais wa Mchezo wa ngumi za Ridhaa Tanzania.

 

Viongozi hao wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika sekta ya Sanaa na Michezo ili kuendelea kuitangaza Tanzania kimataifa.

 

Aidha, Katibu Mkuu Bw. Yakubu amewahimiza viongozi hao kuwaandaa washiriki vizuri tayari kwa mashindano wanayoshiriki ili kujihakikishia ushindi na kufanya vizuri katika mashindano ya ndani ya nchi na ya kimataifa.

No comments:

Post a Comment