MKURUGENZI MKUU NSSF ABAINISHA SABABU ZA KUCHELEWA KUKAMILIKA HOTELI YA KITALII YA NYOTA 5 JIJINI MWANZA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 15 June 2023

MKURUGENZI MKUU NSSF ABAINISHA SABABU ZA KUCHELEWA KUKAMILIKA HOTELI YA KITALII YA NYOTA 5 JIJINI MWANZA

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii ( NSSF) Masha Mshomba, akitoa maelezo kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuhusu ujenzi wa mradi wa hoteli ya kitalii ya nyota tano inayomilikiwa na NSSF iliyopo jijini Mwanza, ambapo alisema ujenzi huo unatarajia kukamilika ifikapo mwezi Juni 2024 baada ya kupatikana muendeshaji wa hoteli mwishoni mwa mwezi huu.

Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza mara baada ya kupokea maelezo kuhusu ujenzi wa hoteli ya kitalii ya nyota tano inayomilikiwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambapo alipongeza NSSF kwa mradi wa hoteli hiyo.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi (kushoto) akitoa maelezo kwa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu taratibu za kupitisha miradi mbalimbali ambayo hupitia Benki kuu ya Tanzania (BOT) ili ishauri na ofisi ya Waziri Mkuu inasimamia na kuwa lengo kuu la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ni kuwekeza kulinda fedha za mifuko.


Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisalimiana na viongozi na wageni mbalimbali alipotembelea ujenzi wa mradi wa hoteli ya kitalii ya nyota tano inayomilikiwa na NSSF iliyopo eneo la Capripoint, jijini Mwanza.

Picha anuai za ukumbusho kwenye eneo la ujenzi wa mradi wa hoteli ya kitalii ya nyota tano inayomilikiwa na NSSF iliyopo eneo la Capripoint, jijini Mwanza.

Picha ya ukumbusho na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipotembelea ujenzi wa mradi wa hoteli ya kitalii ya nyota tano inayomilikiwa na NSSF iliyopo eneo la Capripoint, jijini Mwanza.

Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisalimiana na viongozi na wageni mbalimbali alipotembelea ujenzi wa mradi wa hoteli ya kitalii ya nyota tano inayomilikiwa na NSSF iliyopo eneo la Capripoint, jijini Mwanza.

Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisalimiana na viongozi na wageni mbalimbali alipotembelea ujenzi wa mradi wa hoteli ya kitalii ya nyota tano inayomilikiwa na NSSF iliyopo eneo la Capripoint, jijini Mwanza.

Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisalimiana na viongozi na wageni mbalimbali alipotembelea ujenzi wa mradi wa hoteli ya kitalii ya nyota tano inayomilikiwa na NSSF iliyopo eneo la Capripoint, jijini Mwanza.

Meneja Usimamizi wa Miradi NSSF, Mhandisi Helmes Pantaleo akitoa maelezo kwa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri  wa Muungano wa Tanzania namna mradi wa hoteli ya kitalii ya nyota tano utakavyokuwa. Mradi huo una ghorofa 16, vyumba 168 vya kulala vya aina mbalimbali ikijumuisha sehemu ya kupumzikia Rais (Presidential Suite), migahawa, sehemu za vinywaji na michezo (sports bar).

NA MWANDISHI WETU, MWANZA

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba, amebainisha mbele ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, changamoto kubwa iliyosababisha  kuchelewa kukamilika mradi wa ujenzi wa hoteli ya kitalii ya nyota tano iliyopo jijini Mwanza eneo la Capripoint inayomilikiwa na NSSF kwamba ni kutokuwepo kwa muendeshaji hoteli wa kimataifa.

Mshomba amesema hayo mbele ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyetembelea mradi huo tarehe 14 Juni, 2023. Hata hivyo amebainisha kuwa kuanzia mwezi Juni mwaka 2024 hoteli hiyo inatarajiwa kukamilika na kuanza kazi rasmi.

Alisema katika uzoefu walioupata kwa wenzao wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya nchi Jirani ikiwemo Afrika Kusini, Zambia na Zimbabwe ni kwamba huwezi kumalizia hoteli ya nyota tano kabla hujapata muendeshaji wa hoteli.

“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia vile hatukupata muendeshaji wa hoteli kipindi kile ndio maana mradi ulishindikana kukamilika,” alisema Mshomba.

Alisema ilipofika mwaka 2017/18, Mfuko ulitangaza zabuni ya muendesha hoteli hata hivyo hakupatikana kutokana na mazingira ya kipindi hicho na mwaka 2019 mwezi Septemba walienda nchini Zambia na Afrika Kusini ili kupata uzoefu jinsi Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya nchi hizo inavyopata waendeshaji wa hoteli ambapo NSSF ilipata kampuni ya Hilton Hotels Worldwide, Radissons Hotels na Legacy Hotel.

Mshomba alisema ilipofika mwezi Machi 2021, shughuli za ujenzi ziliendelea na  walianza kumtafuta msanifu wa kuandaa michoro na mahitaji muhimu kwa ajili ya kumalizia kazi za ndani kwa viwango vya kimataifa (interior designer Architect) M/s SOURCE IBA toka Afrika Kusini. 

Alisema mwezi Septemba 2022 walitangaza zabuni ya kumpata muendesha hoteli wa kimataifa, na kwamba kipindi hicho zile kazi ambazo zinahitajiwa kuendelea kabla ya kuwa na muendesha hoteli zilikuwa zinaendelea kama vile ujenzi wa vyoo na madirisha.

Mshomba alisema mpaka sasa baada ya kutangaza zabuni wamewapata  waendesha hoteli watatu ambao waliomba zabuni ikiwemo kampuni ya Hilton Hotels Worldwide, Radissons Hotels na Legacy Hotel, ambapo mwishoni mwa mwezi huu wanatarajia kupata mshindi.

Alisema baada ya kupatikana kwa muendesha hoteli, wanatarajia hadi kufika mwezi Juni 2014 ujenzi wa hoteli hiyo uwe umekamilika na kwamba itachangia sana shughuli za kitalii jijini Mwanza.

Aidha, ameomba  kukamilika kwa mradi wa hoteli hiyo kuende sambamba na kuendeleza uwanja wa ndege wa Mwanza.

“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ni vema jambo hili likaenda sambamba na kuendeleza uwanja wa ndege wa Mwanza maana yake watu watakapokuja kutalii watahitaji kulala katika hoteli hii ya nyota tano,” alisema Mshomba.


No comments:

Post a Comment