TMA YAONGOZA VIKAO KUIDHINISHA TAARIFA YA SITA YA TATHMINI YA MABADILIKO YA HALI YA HEWA NA TABIANCHI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 25 March 2023

TMA YAONGOZA VIKAO KUIDHINISHA TAARIFA YA SITA YA TATHMINI YA MABADILIKO YA HALI YA HEWA NA TABIANCHI

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Ladislaus Chang’a, ambaye pia ni Afisa Kiungo wa Tanzania katika Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (Intergovernmental Panel on Climate Change - IPCC) akiongoza vikao vya kamati ya jopo hilo (Contact Group) katika mkutano wa 58 wa IPCC (Fifty-Eighth Session of the Intergovernmental Panel on Climate Change – IPCC 58), uliofanyika Interlaken, Uswisi kuanzia tarehe 13 hadi 18 Machi, 2023.Pamoja naye ni, Bi. Tina Christensen kutoka Denmark.

Vikao vya kamati ya jopo hilo (Contact Group) katika mkutano wa 58 wa IPCC (Fifty-Eighth Session of the Intergovernmental Panel on Climate Change – IPCC 58), uliofanyika Interlaken, Uswisi vikiendelea.

KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Ladislaus Chang’a, ambaye pia ni Afisa Kiungo wa Tanzania katika Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (Intergovernmental Panel on Climate Change - IPCC) ameongoza vikao vya kamati ya jopo hilo (Contact Group) katika mkutano wa 58 wa IPCC (Fifty-Eighth Session of the Intergovernmental Panel on Climate Change – IPCC 58), uliofanyika Interlaken, Uswisi kuanzia tarehe 13 hadi 18 Machi, 2023.

Jopo la IPCC lilikutana kwa lengo kuu la kuidhinisha Taarifa ya Sita ya Tathmini ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi “IPCC Synthesis Report of the Sixth Assessment cycle (AR6) - Climate Change 2023". Utaratibu wa kuidhinisha taarifa za tathmini za IPCC uhusisha kamati ambazo huteuliwa kufanya mapitio ya maeneo maalumu katika rasimu ya taarifa na kutoa mapendekezo. Kwa upande wake, Dkt. Chang’a, aliteuliwa kuongoza kamati ya kuidhinisha “Sehemu A” ya taarifa hiyo (Section A and Figures, Summary for Policymakers of the Working Group III Contribution to the IPCC Sixth Assessment Report –SPM 1 and the associated Figure Caption) akishirikiana na Bi. Tina Christensen kutoka Denmark. Sambamba na kuongoza kamati hiyo, Dkt. Chang’a alitoa mchango wa kitaalamu wa sayansi ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi kwa Tanzania katika taarifa hiyo kwa manufaa ya nchi yetu na hivyo kuitangaza vyema Tanzania Kimataifa.

Katika hatua nyingine, Dkt. Chang’a alikutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Taasisi ya Hali ya Hewa ya Korea (Korean Meteorological Adminstration – KMA) kuhusu ushirikiano na TMA katika masuala ya hali ya hewa ambapo kiongozi huyo alisema KMA iko tayari kupanua wigo wa ushirikiano na TMA. Miongoni mwa maeneo ambayo walikubaliana KMA na TMA kushirikiana ni matumizi ya mifumo ya kiditajitali katika uandaaji wa utabiri wa hali ya hewa,ufungashaji na usambazaji wa taarifa za hali ya hewa.

No comments:

Post a Comment