PIC YARIDHISHWA UJENZI DARAJA LA JPMAGUFULI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya

Saturday, 25 March 2023

PIC YARIDHISHWA UJENZI DARAJA LA JPMAGUFULI

Mhandisi Abdulkarim Majuto mshauri wa mradi wa daraja la JPMagufuli akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), walipokagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo lenye urefu wa KM 3 Mkoani Mwanza.

Katibu Mkuu Sekta ya Ujenzi Balozi, Eng. Aisha Amour akimuongoza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Mhe. Jerry Silaa pamoja na Kamati yake kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la JPMagufuli lenye urefu wa KM 3 Mkoani Mwanza. 

Muonekano wa daraja la JPMagufuli (Kigongo-Busisi Km 3), Mkoani Mwanza ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 70 na linatarajiwa kukamilika mwezi Februari mwakani.

Mhandisi Abdulkarim Majuto mshauri wa mradi wa daraja la JPMagufuli akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), walipokagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo lenye urefu wa KM 3 Mkoani Mwanza.

Mhandisi Abdulkarim Majuto mshauri wa mradi wa daraja la JPMagufuli akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), walipokagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo lenye urefu wa KM 3 Mkoani Mwanza.

Muonekano wa daraja la JPMagufuli (Kigongo-Busisi Km 3), Mkoani Mwanza ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 70 na linatarajiwa kukamilika mwezi Februari mwakani.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Mhe. Jerry Silaa amesema kamati yake inaridhishwa na kasi ya ujenzi wa daraja la JPMagufuli maarufu Kigongo-Busisi lenye urefu wa kilometa tatu na barabara unganishi kilometa 1.66.

Mhe. Silaa amesema uwekezaji katika daraja hilo ni uwekezaji sahihi kwani litafungua huduma za uchukuzi kati ya Kenya, Tanzania na Uganda kupitia Sirari-Musoma-Mwanza-Geita,Bukoba hadi Mutukula nchini Uganda.

“Zaidi ya shilingi bilioni 700 zimewekezwa ili kuwezesha sehemu ambayo sasa wananchi wanatumia saa mbili kuvuka kwa kutumia vivuko, daraja likikamilika, watatumia dakika nne”, amesisitiza Mhe. Silaa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Sekta ya Ujenzi Balozi, Eng. Aisha Amour ameishukuru Kamati ya PIC kwa ushauri na miongozo kwa Wizara na kuihakikishia kuwa Wizara itasimamia kikamilifu ujenzi wa daraja hilo ili likamilke kwa wakati na ubora uliokusudiwa.

“Hatutamwongeza mkandarasi muda hivyo ajitahidi akamilishe kwa wakati na ubora kama mkataba unavyoelekeza”, amesisitiza Balozi, Eng. Aisha Amour .

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Rogatus Mativila amesema daraja hilo linalojengwa na kampuni ya M/s China Civil Engineering Construction Cooporation (CCECC), limetoa ajira zaidi ya elfu moja na asilimia 94.3 ya ajira hizo zikiwa za watanzania.

Daraja hilo lenye urefu wa KM 3 litakapokamilika litakuwa daraja refu kuliko yote Afrika Mashariki na la sita kwa urefu barani Afrika likitanguliwa na madaraja ya 6th October Bridge  la Misri  KM 20.5, Third Mainland Bridge la Nigeria KM 11.8 , Suez Canal Bridge la Misri KM 3.9, Mozambique Island Bridge la Msumbiji KM 3.8 na Dona Ana Bridge la Msumbiji KM 3.67

IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI.

No comments:

Post a Comment