MURTAZA MANGUNGU Murtaza ASHINDA UENYEKITI SIMBA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday 30 January 2023

MURTAZA MANGUNGU Murtaza ASHINDA UENYEKITI SIMBA

MURTAZA MANGUNGU (Pichani) aliyekuwa mwenyekiti wa Simba SC ameshinda tena nafasi hiyo baada ya kuchaguliwa na wajumbe wa mkutano Mkuu wa SSC uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Murtaza amemshida mpinzani wake kwa kupata jumla ya kura  1,311. 

Murtaza Mangungu ameshinda uchaguzi nafasi ya Mwenyekiti wa Klabu kwa kupata kura 1,311.

Bw. Mangungu amemshinda mpinzani wake, Adv. Moses Kaluwa aliyepata jumla ya kura 1045 katika uchaguzi huo.

Kwa upande wa wajumbe 5 walioshinda nafasi ya ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ni;-

1. Dr Seif Ramadhan Muba - kura 1636

2. Asha Baraka - kura 1564

3. CPA Issa Masoud Iddi - kura 1285

4.  Rodney Chiduo - kura 1267

5.  Seleman Harubu - kura 1250

#SimbaAGM2022 #NguvuMoja

No comments:

Post a Comment