MHE. GEKUL ASISITIZA MAZOEZI KILA JUMAMOSI YA MWISHO WA MWEZI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday 11 December 2022

MHE. GEKUL ASISITIZA MAZOEZI KILA JUMAMOSI YA MWISHO WA MWEZI


Na Shamimu Nyaki

NAIBU Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Pauline Gekul amesisitiza jamii kutekeleza Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kufanya mazoezi  kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.

Mhe. Gekul amesema hayo wakati alipokua Mgeni Rasmi  kwenye mashindano ya mbio mjini Moshi ya Mr UK Marathon yaliyofanyika Wilayani hapo Desemba 11, 2022 Mkoani Kilimanjaro, na  kusisitiza kuwa mazoezi yanaimarisha afya, yanajenga uhusiano na upendo.

"Nawasisitiza Wananchi kuendelea kutekeleza agizo la Mhe. Rais Mama Samia la kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zetu na kujikinga na maradhi yasioambukiza, ili tuwe na Afya njema tuweze  kufanya  shughuli za kuongeza kipato cha Jamii na Taifa letu" amesisitiza Mhe. Gekul.

Mhe. Gekul amewaasa Wandaaji wa Marathon mbalimbali na mabonanza nchini kushirikisha  Wazee, Walemavu, na Watoto ili nao washiriki kama ilivyo kwa vijana kwa sasa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini Mhe. Abbasi Kayanda amesema marathon hiyo, imesaidia Wananchi wa Moshi kuhamasika kufanya mazoezi, lakini pia imeinua uchumi wao, na kutoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kufanya mabonanza mengine ya michezo.

Marathon hiyo imeshirikisha mbio za KM 10, 5 na 2 kwa wanaume na wanawake, ambapo washindi wamepatiwa Medali na zawadi mbalimbali.


No comments:

Post a Comment